loader
Picha

Bandari kavu kujengwa Inyara

SERIKALI imesema inatarajia kujenga bandari kavu katika eneo la Inyara wilayani Mbeya kuondoa kero ya ucheleweshaji wa mizigo inayokwenda nchi jirani.

Mpango huo unatarajiwa kuinufaisha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) kwa kuingia mikataba na nchi hizo na wafanyabiashara kusafirisha bidhaa badala ya kutumia barabara.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema hayo alipokuwa akizungunza na wafanyakazi wa Forodha katika eneo la Tunduma mkoani Songwe, mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Amesema, kwa sasa kumekuwa na ucheleweshaji wa mizigo inayokwenda Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo, jambo ambalo huwachukua siku saba kufikia walengwa kutokana na umbali mrefu wa usafirishaji kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi Tunduma.

Alisema kuwa bandari kavu ya Inyara itakuwa chini ya Mamlaka ya bandari nchini(TPA), hivyo mizigo ikiagizwa kwa nchi za kusini, itapokewa katika bandari ya Inyara hivyo kupunguza umbali wa kufikisha mizigo kwa wahusika.

"Biashara nyakati hizi ni ya ushindani na watu wanajali muda hivyo hakuna anayeweza kusubiri mzigo kwa siku saba," amesema.

Kamwelwe alisema pia kuanzishwa kwa bandari kavu ni fursa kibiashara kwa Tazara kuweza kuingia mikataba ya usafirishaji na wafanyabiashara wa nchi jirani.

Ofisa Forodha, Daniel Charles alisema changamoto inayowakabili ni magari kuchelewa kuruhusiwa kuingia nchini Zambia kutokana na wingi wa vibali hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari upande wa Tanzania.

Alitaja baadhi ya vibali ambavyo madereva wanatakiwa kuwa navyo kuwa ni ushuru wa barabara, uchafuzi wa mazingira.

WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu katika mgodi mpya wa Ndurutu, Kijiji ...

foto
Mwandishi: Merali Chawe, Mbeya

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi