loader
Picha

Maeneo 65 ya uwekezaji Dodoma

UONGOZI wa Mkoa wa Dodoma ukishirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wameainisha maeneo 65 yenye fursa ya uwekezaji katika halmashauri saba na jiji la Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amesema maeneo yaliyoainishwa ni ya fursa za kuwekeza miradi mikubwa ya kijamii na ya kiuchumi katika halmashauri na jiji zima.

Amesema, maeneo hayo ni 20 yanayofaa kwa ajili ya kuwekeza rasilimali za majengo na nyingine. Pia walibainisha maeneo 14 ya uwekezaji katika kilimo, maeneo 10 yanayofaa kwa ajili ya ujenzi wa taasisi za mafunzo mbalimbali na maeneo saba yanayofaa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

"Lakini pia maeneo sita yanayofaa kwa stendi za mabasi, wakati maeneo mengine sita yanafaa kwa ajili ya uegeshaji malori na maeneo mawili yanafaa kwa ajili ya miradi ya ufugaji," amesema.

Dk Mahenge amesema, mkoa huo unafaa kwa ajili ya uwekezaji katika maeneo hayo kutokana na ardhi, hali ya hewa na uoto wa asili rafiki kwa watakaotaka kuwekeza katika mkoa huo.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alisema wamejiandaa kukaribisha wawekezaji kwa kupima viwanja vya kutosha kwa uwekezaji katika maeneo mbalimbali.

"Wawekezaji wasisite kuwekeza Dodoma kwani miundombinu inaboreshwa kuhakikisha wawekezaji hawapati tabu kwenye maeneo yaliyoainishwa mkoani humo," amesema.

WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu katika mgodi mpya wa Ndurutu, Kijiji ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi