loader
Picha

Leseni za madereva wote kukaguliwa

KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Babarani Tanzania, Fortunatus Muslimu amesema kuanzia Agosti Mosi, leseni za madereva wote nchini zitahakikiwa.

Amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, uhakiki utaanzia kwa madereva wa magari ya abiria, watafuata wa mizigo, wa pikipiki, madereva wa magari binafsi na mwisho wa magari ya serikali.

Kwa mujibu wa kamanda Muslimu, fomu za uhakiki huo zitasambazwa nchi nzima kwenye vituo vya mabasi, mizani na kwa matrafiki barabani.

Ametoa wiki moja kwa madereva wote wanaodaiwa faini za makosa ya usalama barabarani yaliyoandikwa kielektroniki kulipa madeni hayo.

Amesema, kuanzia Agosti Mosi utaanza msako mkali na kwamba, madereva wote ambao hawajalipa faini hizo watakamatwa na kushitakiwa mahakamani, na magari yao yatapelekwa Polisi kikosi cha usalama barabarani.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameshtushwa na taarifa za imani za ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi