loader
Picha

Serikali kuimarisha soko la chumvi

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema wizara yake inaangalia namna bora ya kuimarisha soko la chumvi inayozalishwa nchini, yenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya ndani na ziada, kwa kuzuia ile inayoingizwa kutoka nchi za nje.

Nyongo amesema hayo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya kutembelea mgodi wa kuzalisha chumvi wa kampuni ya Stanley and Sons ulioanzishwa mwaka 1948/49 uliopo katika Kijiji cha Kitame wilayani humo.

Akizungumzia uzalishaji chumvi, Nyongo ametoa mfano wa mgodi pekee wa Stanley kuwa huzalisha chumvi kati ya tani 4,000 hadi 6,000 kwa mwaka kulingana na hali ya hewa, licha ya kuwepo migodi mingi ya uzalishaji chumvi katika baadhi ya mikoa nchini ambapo mara nyingi wazalishaji wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa soko la chumvi wanayozalisha.

Alitaja baadhi ya mikoa yenye migodi ya kuchimba na kuzalisha chumvi kuwa ni Pwani yenye zaidi ya mgodi mmoja, Kigoma eneo la Uvinza, Lindi na Mtwara.

Amesema, chumvi ni bidhaa mtambuka inayotumika kama chakula, dawa na ni madini, hivyo aliwataka wachimbaji na wazalishaji wa chumvi kusindika chumvi hiyo katika ujazo tofauti na kwa bei nafuu ili kila mmoja aweze kununua kwa matumizi ya nyumbani, viwandani na kwa ajili ya mifugo.

Mmoja wa wakurugenzi katika mgodi wa chumvi wa Kampuni ya Stanley and Sons, Richard Stanley ameiomba serikali kuboresha miundombinu ya barabara itakayorahisisha usafirishaji ya chumvi hiyo.

ILI Tanzania ijenge Uchumi wa Viwanda, hadi kufikia mwaka 2025 ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Bagamoyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi