loader
Picha

Leseni za madereva wote kuhakikiwa

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limetangaza kuanza operesheni ya uhakiki wa leseni za madereva wote nchini inayotarajiwa kuanza Agosti mosi mwaka huu, huku madereva 173 nchini wakiwa wamefikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali kuhusu leseni za udereva.

Pia Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kimesema kimekusanya zaidi ya Sh bilioni mbili kama tozo ya makosa ya usalama barabarani kuanzia Juni mosi hadi Juni 30 mwaka huu.

Taarifa hizo zimetolewa na maofisa Polisi wa ngazi tofauti nchini katika mikutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Fortunatus Musilimu amesema, kwamba uhakiki huo utaanzia kwenye magari ya kubeba abiria na kutakuwa na fomu maalumu ambazo zitakuwa katika ofisi za wakuu wa usalama barabarani pamoja na vituo vya mabasi ambayo itajazwa taarifa za dereva, madaraja ya leseni, chuo au shule aliyosoma kabla ya kupata leseni.

“Tunaomba wakati wa uhakiki madereva waende na leseni na vyeti halisi vya chuo na shule aliyosoma na madereva watakaobainika kuwa na leseni bila vyeti vya vyuo au shule walivyosoma leseni zao zitazuiliwa na watalazimika kwenda darasani kusoma kabla ya kutahiniwa na kufaulu na kurejeshewa leseni zao,”alisema Musilimu.

Musilimu alisema kabla ya kuanza kwa uhakiki huo tayari walishaanza uhakiki wa leseni za madereva kwa kipindi cha kuanzia Julai nne hadi 15 na jumla ya leseni 73,904 zilikaguliwa na kati ya leseni hizo madereva 878 walibainika kuendesha magari wakiwa na leseni zenye madaraja yasiyostahiki.

Aidha, alisema leseni 225 za madereva zilikamatwa na zimezuiliwa kutokana na madereva wenye leseni hizo kutokuwa na vyeti vya vyuo au shule walizosoma kabla ya kupata leseni na jumla ya leseni 1,808 zilikamatwa kutokana na madereva kuzitumia wakati zimemalizika muda wake.

Wakati huo huo, jumla ya magari 133 yameondolewa barabarani na yatafutiwa usajili kwa mujibu wa sheria baada ya kubainika kuwa mabovu kiasi cha kuhatarisha usalama.

Aidha jumla ya magari 1, 172 yamezuiliwa na kung’olewa namba ili yakafanyiwe matengenezo na kurejeshwa kwa ukaguzi wa mara ya pili kabla ya kuruhusiwa tena kutembea barabarani.

Kamanda Musilimu alisema katika ukaguzi wa vyombo vya moto jumla ya vyombo vya moto 81,533 vimekaguliwa yakiwemo mabasi 4,068, malori 10,643, kosta 9,473, hiace 7,327 , noah 2,138, taxi 1,925, magari binafsi 22,421 , pikipiki 6,678 na bajaj 16,860 zilikaguliwa.

Aliongeza kuwa kati ya vyombo hivyo vilivyokaguliwa, jumla ya magari 48,896 yalikuwa mazima na magari 33,637 yalikuwa mabovu.

Aidha jumla ya madereva 154 wamefikishwa mahakamani kwa kuendesha magari mabovu barabarani na jumla ya wamiliki 25 wamefikishwa mahakamani kwa kuruhusu mgari mabovu kuendeshwa barabarani.

Katika mkutano mwingine hapo jana Kamanda wa Polisi Kanda, Lazaro Mambosasa alisema bilioni 2 zilizoingia katika mfuko wa serikali zimetokana na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya usalama barabarani ambapo jumla ya magari 42,488 yalikamatwa, pikipiki 1,941, daladala 21,946, magari mengine Aidha Mambosasa alisema jumla ya waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda 73 watafikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu ‘helmet’ na kupakia abiria zaidi ya mmoja maarufu kamamishikaki.

Kwa habari zaidi pitia

https://youtu.be/GKcT8QcYL4U

https://youtu.be/A_x4ycZAxd8

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameshtushwa na taarifa za imani za ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi