loader
Picha

Sabasaba vunja bei kila wiki

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade) inaanzisha soko lijulikanalo 'Soko la Sabasaba Vunja Bei Bonanza’ kila Jumamosi na Jumapili kuanzia Julai 28, mwaka huu, lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kununua bidhaa zenye punguzo la bei.

Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Edwin Rutageruka amesema Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu soko litakalofanyika katika viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Amesema soko hilo ni ubunifu wao kuwezesha wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa pamoja na wenye viwanda kufanya biashara ili wapate soko endelevu la bidhaa na wananchi wanufaike na punguzo kupitia bidhaa hizo.

Alisema pia wanawaalika wafanyabiashara wa nje kushiriki katika soko hilo, ilimradi wafanyabiashara wote watoe bei maalumu zenye punguzo.

Kwa upande mwingine alisema, kwenye soko hilo kutakuwa na michezo na burudani mbalimbali ambayo itatoa burudani kwa watoto na watu wazima, pamoja na nyama choma.

Alisema hadi kufikia jana tayari kampuni 108 za hapa nchini zilikuwa zimejiandikisha kwa ajili ya kuuza bidhaa zao, lakini bado wanaendelea kupokea maombi kwa wahitaji. 

Meneja wa Mradi huo wa ‘Vunja Bei Bonanza,’ Samsonite Odera amesema, walitumia miaka miwili kutengeneza mifumo ya mradi huo, kwa kuwa waliona imefika mahali pa kutengeneza mifumo ya wafanyabiashara kupata nafasi ya soko la pamoja.

ILI Tanzania ijenge Uchumi wa Viwanda, hadi kufikia mwaka 2025 ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi