loader
Picha

CCM yamjia juu Lugola kuhusu bodaboda

KATIBU Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kutafakari utendaji wa polisi kutokana na kuongezeka kukamatwa kwa bodaboda zilizojazana vituo vya polisi bila sababu za msingi.

Akizungumza katika mikutano ya kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, amesema lazima vitendo vya kukamata bodaboda na kuwanyanyasa madereva wake vikomeshwe.

Alisema ni lazima polisi wafanye kazi kwa kutenda haki na kuzingatia utu wa watu maana katika baadhi ya maeneo unyanyasaji wa waendeshaji bodaboda umekuwa wa kiwango cha juu na kuumiza wasio na hatia.

“Hatutaki kuwatetea waendesha bodaboda, lakini tunataka polisi wazingatie haki na utu, namtaka Waziri wa Mambo ya Ndani kufanyia kazi suala hilo kuondoa vitendo vya udhalilishaji na uonevu kwa bodaboda,” alisema Katibu Mkuu wa chama hicho kinachounda serikali.

Hoja za Nape Katika hatua nyingine, Dk Bashiru amesema utukutu na hoja zinazoibuliwa na wabunge Nape Nnauye wa Mtama na Hussein Bashe wa Nzega Mjini, ni muhimu katika kuibua mijadala ndani ya chama hicho.

Dk Bashiru akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kakonko juzi, alisema utukutu na utundu wa wabunge hao ni muhimu kwa CCM katika kukifanya kuwa hai katika kuibua mijadala inayogusa jamii.

Hata hivyo, alisema ni lazima suala hilo lifuate taratibu na kuwa na nidhamu wakati wa kuibua na kushughulikia mijadala hiyo, na ni lazima wanaCCM wajenge kujiamini kunapoibuka mijadala inayoibuliwa na vijana kama hao.

“Si vyema kuwaziba mdomo watu wanaoibua mijadala ndani ya CCM wala siyo vizuri kuwaona kuwa ni wasaliti, mijadala hiyo inajenga na kupanua fi kra za wanaCCM katika kufi kiria mambo kwa upana wake, lakini utovu wa nidhamu wakati wa mijadala hiyo haitapewa nafasi na watakaofanya hivyo tutawaadhibu,” alisema Dk Bashiru.

Matumizi ya wasanii Wakati huohuo, chama hicho kimesema kuanzia sasa hakitawatumia wasanii na kuzunguka nao katika maeneo mbali mbali nchini kwenye kampeni na shughuli zake nje ya chama, badala yake TOT itabaki kuwa kikundi pekee cha burudani cha chama tawala.

Dk Bashiru alisema hayo katika uzinduzi wa kampeni ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, ambako CCM imemsimamisha Christopher Chiza. Badala yake, Dk Bashiru ameitaka CCM ngazi ya mikoa na wilaya kuunda vikundi vya sanaa na utamaduni vitakavyotumika kwenye kampeni na shughuli za chama badala ya kuagiza wasanii kutoka mbali na maeneo yao.

Aidha, Katibu Mkuu huyo ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuweka utaratibu wa kuanzisha programu za masomo ya sanaa na utamaduni shuleni ili kuibua vipaji vya wanafunzi.

Alisema Tanzania imejaaliwa kuwa na vipaji kwa vijana wadogo hivyo ni lazima vipaji hivi kuanza kuibuliwa mapema na kuwekewa misingi ya kuendelezwa ili kupata wasanii mahiri siku za baadaye.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameshtushwa na taarifa za imani za ...

foto
Mwandishi: Na Fadhili Abdallah, Kigoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi