loader
Picha

Wema Sepetu, Nature kumuaga Canavaro

WASANII wakiwemo mwigizaji Wema Sepetu, Msaga Sumu, Juma Nature wanatarajiwa kumuaga beki na nahodha mkongwe wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro ' katika bonanza la michezo litakalofanyika Agosti 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Akizungumzia bonanza hilo Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema kutakuwa na mechi itakayochezwa saa 8.00 mchana kati ya timu ya wanawake ya Yanga Princess dhidi ya Kombaini ya Morogoro itakayosimamiwa na mhamasishaji Sepetu.

Alisema saa 10:00 jioni kutakuwa na mechi kati ya Yanga dhidi ya timu ya Ligi Daraja la Kwanza ya Mawenzi yenye wachezaji wengi waliowahi kucheza na Canavaro, akiwemo Abdi Kassim 'Babi' na wengine.

"Tumealika wasanii mbalimbali kama Billnas, Lulu Diva, Gigy Money, Mr. Bluu, Msaga Sumu, Doro Richeon kutoa burudani ya kumuaga Canavaro. Tunawaomba wanachama na mashabiki kujitokeza kwa wingi kusherehekea, "amesema na kuongeza kuwa, mechi hiyo itakuwa pia ni sehemu ya maandalizi ya ligi na michuano ya kimataifa.

Amesema siku hiyo itajulikana mchezaji mrithi wa jezi ya Canavaro namba 23. Viingilio vya mchezo huo ni Sh 10, 000 kwa VIP na 5,000 kwa viti vya kawaida.

WAKATI Klabu ya Simba wakidhamiria kumpeleka mwanachama wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi