loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri azitaka kampuni za uwindaji zichangie zaidi

WAZIRI wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amezitaka kampuni za uwindaji wa kitalii nchini kuongeza michango ya fedha na huduma kwa jamii inayozunguka mapori ya akiba nchini.

Akizungumza na watendaji wa Taasisi ya uhifadhi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) inayomiliki kampuni za uwindaji wa kitalii, katika maonesho ya Nanenane kitaifa mkoani Simiyu, Dk Tizeba amesema kuna kampuni zinapata fedha nyingi lakini uchangiaji jamii ni ndogo.

"Nyie najua mnafanya vizuri lakini wenzenu katika maeneo mengine hadi wamefikia hatua ya kuwachagulia miradi wananchi," amesema.

Ofisa Uhusiano wa FCF, Clarence Msafiri amesema kampuni zilizo chini ya taasisi hiyo zimekuwa zikitoa kwa jamii asilimia 20 ya mapato yao kila mwaka.

Alisema kampuni zao ikiwepo Mwiba Holding na TGTS na walizowekeza wilayani Meatu pori la Akiba la Maswa na Makao, licha ya kutoa michango ya kijamii pia kwa mwaka wanatoa kwa vijiji zaidi ya Sh milioni 610 kama kodi ya pango.

Meneja ujirani Mwema wa kampuni ya Mwiba Holdings, Alfred Mwakivike alisema kampuni hiyo kabla ya kusaidia miradi imekuwa ikipata maelekezo ya halmashauri.

Alisema miradi wanayoitekeleza ina thamani zaidi ya Sh bilioni mbili na yote imeidhinishwa na Halmashauri ya Meatu.

Taasisi ya Friedkin inashiriki Maonesho ya Nanenane kwa mara ya kwanza kuhamasisha uhifadhi, kupiga vita ujangili na pia kuonesha umuhimu wa uhusiano wa uhifadhi na kilimo.

KUANZIA sasa wafanyabiashara nchini na nchi ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi, Bariadi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi