loader
Picha

Wazalishaji watakiwa kuthibitisha ubora wa bidhaa

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa miezi mitatu kwa wazalishaji wa bidhaa zilizo katika orodha ya viwango vya lazima kutakiwa kuthibitishwa ubora wake.

Katika kipindi hicho, shirika litathibitisha ubora wa bidhaa hizo na wasambazaji na wauzaji watatakiwa kuingiza sokoni bidhaa zenye ubora.

Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Ngenya Yusuf alitoa agizo hilo jana katika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu katika uwanja wa Nyakabindi.

Alifafanua kuwa bidhaa zilizo katika viwango vya lazima ni zile zinazoweza kuleta athari za kiafya, kiusalama ama kuharibu mazingira.

Alitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na bidhaa za vyakula, vifaa vya ujenzi, vilainishi vya mitambo na bidhaa za petroli.

Dk Ngenya Ngenya alisema hatua hiyo imefikiwa kutokana na baadhi ya wazalishaji kuzalisha bidhaa bila kufuata taratibu za kuthibitisha ubora wake kabla ya kuziingiza sokoni. Alisema kazi ya kuondoa sokoni bidhaa zisizo na ubora Iitaanza ifikapo Desemba mwaka huu.

TBS kwa sasa inaendelea kutoa elimu nchini kote kuhamasisha wazalishaji kuthibitisha ubora wa bidhaa na umma kununua bidhaa zenye ubora, kupitia njia mbalimbali yakiwemo maonesho, matangazo kupitia vyombo vya habari na makongamano.

Kwa upande wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi, Dk Ngenya alisema shirika litaendelea kudhibiti mianya ya uingizaji wa bidhaa hafifu kwa kuimarisha ofisi za mipakani na bandarini.

Alisisitiza kuwa ni jukumu la waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kuhakikisha kuwa bidhaa zao zinakaguliwa na mawakala wa TBS kabla ya kusafirisha kuja nchini.

Alisema kwa kufanya hivyo itasaidia soko la ndani kuwa na bidhaa bora na kulinda viwanda vya nchini na kuleta ushindani ulio sawia.

Wakati huo huo, aliwataka waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kufuata taratibu zilizowekwa na shirika kwa mujibu wa sheria kuepuka hasara ya kurudisha bidhaa zilikotoka ama kuziharibu kwa gharama za muagizaji.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi, Bariadi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi