loader
Picha

El Jadida yambania Msuva

DAU la Sh bilioni 4 linalotakiwa na klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco, linaweza kukwamisha ndoto za Simon Msuva kucheza soka Ulaya.

Akizungumza jana baba mzazi wa Msuva, Happygod Msuva amesema mwanawe anatakiwa na timu nne zikiwemo za Ulaya na nyingine za nchini Morocco, lakini dau la Difaa El Jadida limekuwa likiwakwamisha.

“Kuna timu Msuva anaendelea kufanya nazo mazungumzo ndani ya Morocco na nje ya Morocco, ikiwemo timu kutoka Hispania ili kuweza kumsainisha, lakini tatizo kubwa limekuwa kwa klabu yake, lakini siwezi kuziweka wazi hizo timu hadi mipango itakapokamilika,” alisema.

“Difaa El Jadida inahitaji karibu Sh bilioni 4 za Kitanzania dau ambalo ni kubwa hivyo anaendelea na mazungumzo na iwapo atafanikiwa, basi anaweza kuondoka wakati wowote kwani ndiyo matarajio yake,” ameongeza mzee Msuva.

Msuva alijiunga na Difaa El Jadida, Julai 29, mwaka jana kwa dau la dola 150,000, sawa na Sh milioni 337 akitokea Yanga na amefanikiwa kuonesha kiwango kiasi cha kuzishawishi timu nyingine hasa zile za Ulaya.

Tangu atue Difaa El Jadida Msuva amekuwa mchezaji pekee wa kigeni katika timu hiyo aliyetoa msaada mkubwa kwa kuifungia mabao mengi kuanzia kwenye Ligi Kuu hadi Ligi ya Mabingwa Afrika na kufanya thamani yake kuongezeka.

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameipongeza timu ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi