loader
Picha

Amunike kocha mpya Stars

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemtambulisha mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, Emmanuel Amunike kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa, Taifa Stars.

Rais wa TFF, Wallace Karia amemtangaza kocha huyo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kusema wamesaini mkataba wa miaka miwili.

Amunike mwenye umri wa miaka 47, aling’ara na Nigeria ‘Super Eagles’ kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1994 iliyofanyika Marekani.

Kocha huyo pia aliisaidia Nigeria kutwaa taji la Afrika mwaka 1994 ilipofanyika Tunisia ambapo pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika.

Kibarua cha kwanza cha Amunike ni kuiongoza Stars dhidi ya Uganda Septemba 8 mwaka huu katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) itakayochezwa Kampala na kisha itacheza na Cape Verde ugenini Oktoba 10 mwaka huu.

Stars inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Lesotho Juni 10 mwaka jana.

Amunike anachukua mikoba ya mzawa Salum Mayanga aliyemaliza mkataba wake Machi 27 mwaka huu ambapo chini yake Stars ilishinda mabao 2-0 mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Congo DR, Machi 27 mwaka huu.

Amunike aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana ya Nigeria chini ya umri wa miaka 17 kwa miaka mitatu, 2014- 2017.

Taifa Stars ndio timu yake ya kwanza ya taifa ya wakubwa kuifundisha. Aliwahi kufundisha klabu kadhaa katika maisha yake ya ukocha zikiwemo Al Hazm mwaka 2008 (Kocha msaidizi), Julius Berger mwaka 2011, Ocean Boys ya Nigeria.

Pia aliwahi kuzifundisha klabu za Al Khartoum SC ya Sudan kwa miaka miwili 2017 na 2018. Nyota huyo alianza kucheza soka katika klabu ya Concord mwaka 1990, Julius Berger 1991 (zote za Nigeria) Zamalek ya Misri mwaka 1991- 1994.

Pia amecheza Ulaya katika klabu za Sporting CP ya Ureno 1994- 1996, Barcelona mwaka 2000, Albacete za Hispania. Mwaka 2003 alisajiliwa na Busan I'Cons ya Korea Kusini kabla ya kuhamia Al-Wehdat ya Jordan mwaka 2004 ambapo huko alistaafu kucheza soka.

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameipongeza timu ya ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi