loader
Picha

Dk. Yonazi aahidi ubunifu kwenye mawasiliano

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dk Jim Yonazi ameahidi kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uaminifu kuhakikisha mawasiliano yanaleta faida kwa umma na Tanzania kwa ujumla.

Akizungumza na HabariLeo siku ya kwanza ofisini kwake katika wizara hiyo jijini Dodoma, Dk Yonazi amesema atafanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wengine wa wizara ili kuhakikisha mawasiliano yanaleta maendeleo ya kiuchumi nchini.

“Nitafanya kazi kwa kushirikiana na wafanyakazi wengine wa wizara kwa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uaminifu na ndicho kitu Watanzania wanataka kutoka kwetu tuliopewa dhamana ya kuwatumikia,” alisema.

Dk Yonazi ambaye aliteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni akitoka nafasi ya Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), alisema anaanza kazi katika wizara hiyo, sekta ya mawasiliano ambayo yeye amekuwa karibu nayo.

Alisema, kabla ya kuanza kazi, amekutana na viongozi mbalimbali wa wizara hiyo, na alitoa ahadi ya kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na watumishi wengine wizarani ili kuhakikisha Watanzania wanakipata wanachohitaji wizara ikifanye kwa ujumla wake.

Kuhusu wajibu wa wizara na hasa sekta ya mawasiliano, Dk Yonazi alisema ina majukumu makubwa ya kuhakikisha inapeleka mawasiliano kwa wananchi, ambayo yanakuwa na faida kwao na kwa nchi hasa mawasiliano salama.

Alisema kama mawasiliano yanakuwa si salama, yanaweza kusababisha hasara kwa wananchi na kwa nchi, hivyo ni wajibu wa wizara katika kuhakikisha wananchi na nchi inakuwa na mfumo wa mawasiliano mazuri na yenye faida kwa serikali na kwa watu binafsi.

Alisema mawasiliano yanatakiwa kuleta faida mfano kwa watu wanaofanya miamala ya kuhamisha fedha kutoka sehemu moja hadi nyingine, yanatakiwa kusaidia wasiibiwe na ifanyike kwa usalama.

“Lakini pia ni wajibu wa wizara kuhakikisha inatoa elimu katika jamii ili wajue umhimu wa habari na kwamba wanatakiwa kutumia habari katika kushiriki katika uchumi wa dunia ambayo unaendeshwa kwa habari,” alisema.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewafi kisha ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi