loader
Picha

Wajasiriamali wahimizwa kuungana wakope

WAKULIMA na wajasiriamali wameshauriwa kujiunga katika vikundi kupata fursa ya mikopo inayotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupitia kampeni yake ya Zamu yako.

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma wakati alipozungumza kwenye maonesho ya Wakulima Nanenane, Viwanja vya Nzuguni Jijini hapa.

Amesema, wakulima na wajasiriamali wakijiunga vikundi watapata fursa ya kunufaika na mpango wa mikopo inayotolewa na mfuko wa NSSF.

"Hatutasaidia mtu mmoja mmoja. Wajiunge katika vikundi iwe rahisi kutambua na kupata mikopo hiyo tunayotoa," amesema Chuma.

Alisema mikopo hiyo haitolewi moja kwa moja na NSSF bali wameingia mkataba na benki za Azania, NMB na benki nyingine za kibiashara.

Aidha alisema kampeni hiyo ni mpango wa hiari unaolenga kuwafikia na kuwaandikisha watu wote waliopo kwenye sekta isiyo rasmi hapa nchini wenye umri kuanzia miaka 18 mpaka 60.

Aliyataja makundi wanayolenga, wajasiriamali, waendesha bodaboda, mamalishe, wakulima na wavuvi ambao wote hao wanatakiwa kujiunga kwenye vikundi vilivyo rasmi vya uzalishaji mali kama Vibindo, Amcos, Vicoba na Saccos.

Alisema uandikishaji unafanyika ofisi zote za NSSF na katika maeneo ya biashara au kazini wakitembelewa na wafanyakazi wa mfuko huo.

Alisema masharti ya mwanachama mpya wa mfuko huo kukidhi vigezo vya kupata mkopo ni lazima awe amechangia kiwango kisichopungua Sh 20,000 kwa mwezi miezi sita mfululizo.

Alitaja faida ya makundi hayo kujiunga NSSF nia kunufaika na mafao ya matibabu bure yeye na wategemezi wanne na fursa ya mikopo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Jackson Masaka aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimsho hayo aliomba kampuni hizo kutoe elimu ya huduma zinazotolewa wazijue.

Masaka ambaye ni mhandisi alisema, taasisi za kifedha zinatakiwa kupunguza masharti ya mikopo wananchi wanufaike na mikopo yao.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewafi kisha ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi