loader
Picha

Simba Day yamalizika kwa sare

SIMBA SC jana ilihitimisha sherehe zake za Simba Day kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana katika mchezo mkali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mchezo huo ulikuwa wa kuhitimisha shamrashamra ya wiki ya Simba zinazofanyika Agosti 8 ya kila mwaka.

Mechi ya jana ambayo Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha gazeti hili, Daily News na SpotiLeo ni mmoja wa wadhamini, ilikuwa nzuri kwa timu zote ambapo zilishambuliana kwa zamu huku kila upande ukionekana kujizatiti katika kila idara.

Simba inayojiandaa kutetea taji lake la Ligi Kuu kuanzia Agosti 22 mwaka huu wachezaji wake walionekana kucheza kwa kuelewana na kama si washambuliaji wake kutokuwa makini kwenye umaliziaji wangepata mabao mengi hasa kipindi cha kwanza.

Mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi alikosa mabao kadhaa katika kipindi hicho kabla Kotoko hawajapata bao la kuongoza katika dakika ya 44. Kotoko waliandika bao hilo kupitia kwa Obed Owuso aliyemzidi maarifa beki wa Simba, Erasto Nyoni.

Bao hilo liliwafanya Kotoko kwenda mapumziko wakiwa mbele, na kuendeleza mashambulizi katika kipindi cha pili. Dakika ya 75, jitihada za Okwi zilizaa matunda kwa kufunga bao la kusawazisha akiunganisha pasi ya Shiza Kichuya.

Mshambuliaji mpya wa timu hiyo, kinda Adam Salamba alikuwa na bahati mbaya jana baada ya mkwaju wake wa penalti kudakwa na kipa wa Kotoko katika kipindi cha pili.

Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi Hance Mabena baada ya Salamba kufanyiwa madhambi na mabeki wa Kotoko akielekea kufungwa.

Mchezaji mwingine mpya wa Simba, Meddie Kagere alifanya mashambulizi matatu ya nguvu jana lakini alishindwa kufunga na dakika ya 63 alitolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Salamba.

Kikosi cha Simba jana: Aishi Manula, Shomari Kapombe/ Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Sergio Wawa, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Cletus Chama, James Kotei/ Hassan Dilunga, Meddie Kagere/ Adam Salamba, Emmanuel Okwi, Shiza

KAMPUNI ya MultiChoice imetangaza kuonesha michezo yote ya michuano ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi