loader
Picha

Chilunda atua Hispania

MAMBO yamekamilika kwa mshambuliaji wa Azam FC, Shaaban Idd ‘Chilunda’ katika dili lake la kujiunga na timu ya CD Teneriffe ya Hispania.

Wiki kadhaa zilizopita Chilunda alisaini mkataba wa miaka miwili na Teneriffe lakini alikwama kujiunga na timu hiyo kutokana na kukosa kibali cha kufanya kazi nchini Hispania.

Taarifa kutoka Azam FC zinasema kuwa mshambuliaji huyo ambaye alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Kagame, alitarajiwa kuwasili Hispania jana asubuhi.

Ratiba yake ilikuwa inaonesha, baada ya kuwasili nchini humo atachukuliwa moja kwa moja na kupelekwa kufanyiwa vipimo vya afya.

Chilunda anakuwa mchezaji wa pili kutoka Azam FC kujiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza Hispania baada ya Farid Mussa kujiunga nayo miwili iliyopita.

WAKATI Klabu ya Simba wakidhamiria kumpeleka mwanachama wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi