loader
Picha

Ridhiwani Kikwete ajivunia viwanda 10 vipya Chalinze

 MBUNGE wa jimbo la Chalinze, wilayani Bagamoyo, Pwani Ridhiwani Kikwete amesema sera ya viwanda inatekelezwa kwa vitendo ili kuwahakikishia Watanzania kuwa serikali ya awamu ya tano imenuia kuwakomboa wanyonge.

Aidha mbunge huyo amesema kuwa jimbo lake kwa sasa lina viwanda zaidi ya kumi na tayari vimekwisha kuanza uzalishaji na vingine vingi vinakuja katika uwekezaji wa aina mbalimbali.

Ridhiwani ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa jitihada zake za kuhakikisha viwanda vinakuwepo nchini kwa lengo la kuzalisha na kuuza ndani na nje ili Watanzania waweze kujiongezea kipato kikubwa zaidi.

Hivyo mbunge huyo amewataka wabunge wenzake kutumia nafasi zao za uwakilishi kwa wananchi kuweza kuwashawishi wawekezaji wa nje na ndani ili wajenge viwanda katika maeneo yao kwani ni fursa kubwa kwa wapiga kura wetu.

Kwa mujibu wa Mzimba Muhamed, mmoja wa wananchi wanaozunguka nma kiwanda hicho, kwa sasa Chalinze ni miongoni mwa majimbo yanayoweza kuongoza katika uwekezaji wa viwanda mbalimbali huku akijinasibu kwa kusema "tuna viwanda zaidi ya 10 na vyote vinafanya kazi za uzalishaji hivyo tunampongeza mbunge wetu kwa juhudi zake za kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza hapa."

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewafi kisha ...

foto
Mwandishi: Shusu Joel

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi