loader
Picha

Maboresho shule za serikali kuongeza ufaulu

SERIKALI imetangaza kuwa maboresho makubwa ya miundo mbinu, mazingira bora ya kujifunza na kufundishia yanayofanywa kwenye shule za sekondari za serikali nchini yataongeza ufaulu wa wanafunzi, imeelezwa.

Pia maboresho hayo yanalenga kuzifanya shule za serikali kuwa na matokeo bora kushindana na shule za binafsi ambazo wazazi wanatumia gharama kubwa kupeleka watoto wao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alipofanya ziara kutembelea Shule Maalumu ya Sekondari ya Kakonko iliyopo wilayani Kakonko mkoani Kigoma na kusema kuwa mpango wa serikali ni kuona shule za sekondari za serikali zinakuwa kwenye 10 bora za matokeo nchini.

Alisema kuwa serilali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza na uboreshaji wa shule kongwe nchini ambapo jumla ya shule 89 zitafanyiwa maboresho makubwa mabapo jumla ya Sh bilioni 89 zitatumika ambapo sambamba na hizo pia maboresho hayo yatafanyika kwa shule za kata.

Katika hilo Waziri Jafo alisema kuwa matokeo ya Kidato cha Sita mwaka huu yamedhihirisha nia ya serikali kuonesha kwa mifano maboresho hayo kutokana na shule nne za serikali kuwa miongoni mwa shule 10 zilizofanya vizuri.

"Tunachotaka ni wananchi kuziona shule zetu za kata kuwa kimbilio maana tunaboresha majengo, tunaleta walimu ili mazingira ya kujifunzia na kufundishia yaweze kuleta uhalisia wa matokeo chanya tunayokusudia.

“Kwa sasa wananchi wanalalamika gharama kubwa ya kupeleka watoto wao kwenye shule nzuri (bora) wanazotaka watoto wao wafaulu vizuri, tukishafika tunapotaka hizo gharama kubwa zitashuka wenyewe maana watu wote watatamani watoto wao wasome shule zetu za kata," alisema Waziri Jafo.

Akiwa shule hapo alieleza kuridhishwa na ujenzi wa mabweni na bwalo la chakula katika shule hiyo na kuwataka wanafunzi kujibidiisha kwenye masomo ili kuendana na mkakati wa serikali wa kuzifanya shule hizo kupata matokeo bora.

Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa majengo katika shule hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko, Lusubilo Mwakabibi alisema kiasi cha Sh milioni 259 zimetolewa kwa ujenzi huo ikiwemo Sh milioni 40 za ujenzi wa maabara ya masomo ya Sayansi na kwa sasa majengo yamekamilika na wanafunzi wanayatumia isipokuwa maabara.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewafi kisha ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi