loader
Picha

Mbaroni wakisafirisha wanafunzi wakawe 'hausigeli'

JESHI la Polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wawili, mwanamke na mwanaume; wakituhumiwa kutaka kuwasafirisha wanafunzi watano wa Shule ya Sekondari ya Mlafi wilayani Kilolo kwenda Dar es Salaam kufanya kazi za ndani.

Wanafunzi hao walitoweka kwa wazazi wao Julai 29, mwaka huu na kusafirishwa kwa bodaboda kutoka kijijini kwao Mlafu hadi Ilula, wakiwa tayari kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amesema watuhumiwa hao walikamatwa Julai 31, mwaka huu wakiwa katika hekaheka ya kuwasafirisha wanafunzi hao.

Bila kutaja majina ya wanafunzi hao, Bwire amewataja watuhumiwa wa uhalifu huo wa biashara ya kusafirisha binadamu kuwa ni Tulizo Mtega (18) na Rosemary Msasalage (18), wote wakazi wa Ilula.

“Mbinu iliyotumika kuwarubuni wanafunzi hao ilikuwa ni kwamba wamepata kazi mbalimbali za kuuza maduka Morogoro na Dar es Salaam,” amesema.

Katika tukio lingine, Kamanda Bwire amesema Agosti 2 saa 10 jioni Jeshi la Polisi lilimkamata Dina Juma (45) mkazi wa Mwangata mjini Iringa, akituhumiwa kumtumikisha kingono mtoto wake wa miaka 14 kwa lengo la kujipatia kipato.

Bwire amesema mtoto huyo amehifadhiwa katika Idara ya Ustawi wa Jamii, baada ya uchunguzi wa daktari kuthibitisha kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo hivyo kwa muda mrefu na hata kulazimishwa anapokataa.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi limesema linawashikilia watu wanane wakituhumiwa kukutwa na mali za wizi katika msako uliofanyika kati ya Julai 31 na Agosti 4, mwaka huu.

Bwire alisema Daniel Mgongolwa (22), Mashaka Lyandala (35) na Faraj Lukosi (30) wakazi wa Semtema na Mkimbizi mjini Iringa walikamatwa wakiwa na mabati 38 ya Afrika Kusini yenye thamani ya Sh milioni moja, mali ya Virginia Chacha.

Rehema Mwampamba (36) na Johari Mnyenyerwa (40) wakazi wa Ipogoro mjini Iringa, walikamatwa wakiwa televisheni flat inchi 28 tatu aina ya LG na nyingine aina Hisense inchi 42 na TCL Inchi 32 na vifaa mbalimbali vya nyumbani, ambavyo baadhi vimetambuliwa na mwenye mali Kurwa Shimiyu mkazi wa Gangilonga, mjini Iringa.

Kamanda Bwire aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Deus Kisonga (29) na Felisi Samweli (28) wakazi wa kijiji ch Ilula wilayani Kilolo, na Frank Mofuga (23) mkazi wa Mtwivila mjini Iringa, waliokamatwa na mali mbalimbali za wizi zikiwemo friji kubwa tatu. Aliwataka watu wanaohisi kuibiwa mali hizo, kujitokeza makao makuu ya jeshi hilo mjini Iringa wakiwa na risiti zao ili kutambua vitu vyao.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewafi kisha ...

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi