loader
Picha

Majeshi yaongoza tuzo Nane Nane

MAJESHI ya ulinzi na usalama kanda ya kati, yameongoza kunyakua tuzo, vikombe na zawadi kwa kufanya vizuri katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika, Nzuguni jijini Dodoma.

Kamati ya maandalizi ya maonesho ya Nane Nane iliendesha mashindano kushindanisha taasisi mbalimbali katika maeneo 25 ambapo majeshi yamechukua nafasi mbili za juu.

Makundi mengine ni watu binafsi wadogo na wakubwa, wajasiriamali, wazalishaji mifugo na wakulima wakubwa na wadogo ambapo majeshi yamefanya vizuri katika makundi na jumla.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ndilo limeibuka mshindi wa kwanza, Jeshi la Magereza limeshika nafasi ya pili na ya tatu ikichukuliwa na Kampuni ya Mbegu (Seed Company).

Akitoa tuzo, vikombe na vyeti washindi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde alipongeza makundi yaliyoibuka washindi hasa majeshi yaliyoongoza.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza katika wafugaji wakubwa ni Kampuni ya Lushu, mshindi wa pili ni Magereza na Kampuni ya Nyama ya Narco iliibuka mshindi wa tatu.

Katika kundi la wafugaji ng'ombe asilia wa nyama, mshindi wa kwanza alikuwa Velentino Masowo aliyekuwa na ng’ombe mwenye uzito wa kilo 948, Assa Yona mwenye ng'ombe wa kilo 859 , Victor Anslem ng'ombe wa kilo 604.

Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa binafsi mshindi alikuwa Nahumu Nassari, mshindi wa pili, Japhet Kayamba na mshindi wa tatu ni Ramadhani Mwanga ambao ng’ombe wao wanatoa maziwa kati ya lita 20-26 kwa siku.

Kwa wafugaji wa ng'ombe wakubwa, mshindi wa kwanza alikuwa Liti Mpwapwa, mshindi wa pili Magereza na hakukuwa na mshindi wa tatu.

Katika tuzo hizo, walikuwapo wakulima bora ambao ni Eliofoo Mwika kutoka halmashauri ya Singida, Mercy Mtei kutoka Jiji la Dodoma na Ramadhan Songo wa Halmashauri ya Kondoa.

Wafugaji bora walikuwa Nahumu Nasoro wa Dodoma, Julius Mpare wa Singida na Velantino Kombo wa Kongwa, wafugaji samaki bora ni Erasmus Msengi wa Iramba, Charles Kidua wa Singida na Manoa Samson wa Chamwino.

Maonesho ya Nane Nane mwaka huu yalikuwa ya 10 kufanyika Nzuguni, ya saba kushirikisha mifugo na kaulimbiu "Wekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewafi kisha ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi