loader
Picha

Wachezaji Simba Sc wamkuna kocha

SARE iliyopata Simba ya bao 1-1 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana si kitu, kilichomkuna Kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems ni namna wachezaji wake walivyocheza kwa kiwango kizuri.

Simba ilicheza mechi ya kirafiki na timu hiyo ya Ghana katika tamasha la Simba Day linalofanyika Agosti 8 ya kila mwaka.

Kocha huyo amesema kiwango cha wachezaji wake kimedhihirisha aliyowafundisha Uturuki walipokwenda kwenye kambi ya mazoezi ya wiki mbili kimeeleweka.

Awali, Aussems amesema, atautumia mchezo huo kuwatazama wachezaji wake kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.

Akizungumza juzi baada ya mchezo huo wa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kocha huyo alisema ameridhishwa na kiwango.

“Nimewaona wachezaji wamecheza vizuri, wameonesha mbinu na ufundi na wametengeneza nafasi nyingi za kufunga, tulimiliki mpira kwa asilimia 75, tunahitaji kuendeleza umoja kufanya vizuri zaidi wakati ujao,” alisema.

Aussems alisema wapinzani wao walikuwa vizuri na zaidi kipa wa Kotoko, Telix Annan ndiye aliyekuwa akivuruga mipango baada ya kuzuia nafasi nyingi zilizokuwa zinaelekezwa golini kwao, ikiwemo kudaka penalti ya Adam Salamba.

Licha ya kudaka penalti hiyo, alisema tabia waliyokuwa nayo wachezaji wake Uturuki imeendelezwa pia katika mchezo huo, jambo linalomfurahisha.

Alisema anataka kuwa na timu inayomiliki mpira, wabunifu, wanaocheza na kutumia nafasi wanazopata.

“Kwa muda wa wiki mbili zilizobaki nitaendelea kuboresha maeneo yaliyokuwa na mapungufu kufanya vizuri zaidi mechi zijazo kwasababu nataka mashabiki wetu wafurahie burudani,” amesema.

Kocha huyo amesema wana mechi tatu za kirafiki Lindi, Mwanza na Arusha ambazo zitazidi kuwaimarisha na kuwaweka tayari kwa ligi.

Aliwaomba mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuendelea kuwaunga mkono katika mechi zao zijazo.

SIMBA inatarajia kutumia jezi za rangi ya kijivu kwenye michuano ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi