loader
Picha

Yanga- Yajayo yatawafurahisha

Yanga yawatoa hofu mashabiki Na Grace Mkojera YANGA imewatoa hofu mashabiki wake kuhusu ubora wa timu yao na kuwaambia mambo mazuri yanakuja.

Mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Bara, wameahidi kufanya vizuri katika michuano ijayo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka huu.

Timu hiyo kwa sasa inaendelea na kambi ya mazoezi Morogoro kujiandaa na msimu mpya sambamba na michuano ya kimataifa.

Akizungumza na gazeti hili jana Mratibu wa Yanga, Hafidh Salehe alisema kikosi kimeanza kurudi katika morali hivyo muunganiko ukikubali watakuwa na timu yenye ushindani mkali.

“Muunganiko ukikubali tu wamekwisha, wachezaji wameanza kuonesha uhai wa timu, wana morali, wanaonyesha juhudi kwenye mazoezi na tunategemea wataendelea hivyo,” amesema.

Salehe alisema kikosi hicho kinajipanga kwa mechi ya majaribio dhidi ya timu ya Ligi Daraja la Kwanza Mawenzi itakayochezwa keshokutwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani humo.

Alisema tayari wamecheza mechi moja ya kimazoezi na wachezaji wameonesha uwezo na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo maalumu wa kumuaga nahodha wao, Nadir Haroub ‘Canavaro’.

Kiongozi huyo aliwataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono kwa vile kuna mambo mazuri yanakuja.

Katika mchezo wa mazoezi waliocheza dhidi ya timu ya kituo cha michezo Tanzanite Morogoro walishinda mabao 5-1 huku mshambuliaji mpya Haritier Makambo akiwasha moto kwa bao moja, mengine yakifungwa na Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Emmanuel Martin na Pius Buswita.

SIMBA inatarajia kutumia jezi za rangi ya kijivu kwenye michuano ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi