loader
Picha

'Acheni kupenda mchezaji, ipendeni Simba SC'

KAIMU Rais wa Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’ amesema umefika wakati wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuweka mapenzi kwa timu na sio mchezaji mmoja mmoja.

Kauli ya kiongozi huyo imekuja kutokana na utamaduni uliojengeka kwa wanachama kumpenda mchezaji mmoja hivyo, asipokuwepo kwenye timu wanaanzisha minong’ono.

Akizungumzia suala hilo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu Haruna Niyonzima kutokuwepo kwenye kikosi kilichotambulishwa, alisema wachezaji wote wana umuhimu, kama mmoja hayupo bado ataendelea kubaki mchezaji wa klabu.

“Wote ni wachezaji wa klabu, hatupaswi kumtizama mtu mmoja kama hayupo timu itaendelea kucheza, tuipende klabu na sio kuangalia labda fulani hayupo ndio basi,” alisema.

Kwenye tamasha la Simba Day juzi, walitambulisha kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu huku jina la Niyonzima likiwa halijatajwa.

Mchezaji huyo wa Rwanda hajatokea tangu timu hiyo ilipoanza mazoezi ya kujifua Uturuki na haijulikani alipo licha ya viongozi wa klabu hiyo kumtaka mapema kujiunga na wenzake kwa maandalizi ya ligi.

Kikosi kilichotangazwa juzi ni Ally Salum, Abdul Suleimani, Rashid Juma, Paul Bukaba, Mohamed Hussein, Said Ndemla, Shomari Kapombe, Muzamiru Yassin, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Nicholas Gyan.

Wengine ni Mohamed Ibrahim, James Kotei, Yusuph Mlipili, Asante Kwasi, Aishi Manula, Deogratius Munishi, Marcel Kaheza, Adam Salamba, Shiza Kichuya, Hassan Dilunga, Paschal Wawa, Mohamed Rashid, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Cletus Chama na John Bocco.

KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi