loader
Picha

Geita wavuka malengo ukusanyaji mapato

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka amesema katika mwaka wa fedha uliopita, halmashauri ilivuka lengo kwa kukusanya asilimia 119 ya mapato kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Ameyasema hayo katika mazungumzo na timu ya waandishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ambayo imejichimbia mkoani Geita.

Amesema walivuka malengo kwa kuongeza nguvu kusimamia mapato katika madini.

Kauli hiyo inafanana na ya Mkurugenzi wa Mji wa Geita, Modest Apolinary aliyesema halmashauri yake imefanya mapinduzi makubwa katika eneo la kukusanya mapato, hatua iliyowawezesha kumudu kutekeleza miradi mingi ya maendeleo.

Alisema walijielekeza ipasavyo katika maeneo ya wafanyabiashara ikiwemo masoko na stendi na kuweka nguvu kwa wachimbaji wa madini na kuhakikisha wanasimamia vyema mapato.

"Wachimbaji madini wa kati, wakubwa na wadogo, wote tumewawekea mfumo mzuri wa ukusanyaji mapato. Ndio maana utaona mwaka 1916/17 tulikusanya zaidi ya Sh bilioni 5.2 na tukatumia asilimia 71 ya mapato yetu yote hayo kwenye miradi ya maendeleo," alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema alipoteuliwa kusimamia mkoa wa Geita alikuta mchango wa wachimbaji wadogo katika uzalishaji wa dhahabu ukiwa asilimia 2 kulinganisha na mgodi wa Geita Gold Mine (GGM).

Amesema aliunda timu yake kuchunguza na kugundua kwamba kulikuwa na usimamizi mbovu wa kile kinachozalishwa huku kukiwa hakuna takwimu za nani anazalisha kiasi gani.

"Kwa hiyo tulikuwa na taarifa ambazo hatuwezi kuzithibitisha. Nikasema, hapana. Tunahitaji kufanya mageuzi makubwa. Unaposhirikiana na ofisi ya madini, ukapima kila kinachozalishwa, unakuwa na uhakika wa mapato," alisema.

Alisema hatua ya serikali kuzuia kaboni ya dhahabu kusafirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, imekuwa faraja kwao na imesaidia kusimamia vizuri mapato ya dhahabu.

Alisema Mei mwaka huu mkoa ulizalisha kilo 20 za dhahabu lakini baada ya katazo na wao kusimamia mapato, Julai takwimu zilionesha kuwa Geita imezalisha kilo 141.3 za dhahabu.

Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita na Halmashauri ya Mji huo wamekiri ongezeko la mapato, mbali ya kuboresha miradi ya jamii, limeongeza kiwango kinachotolewa mikopo kwa vikundi vya akina mama na vijana.

TSN iko mkoani Geita kuumulika mkoa huu na kuandaa Jukwaa la Fursa za Biashara Geita litakalofanyika Agosti 15 na 16, 2018 kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa huo. Tayari makampuni kadhaa yamedhamini Jukwaa hilo litakaloenda sambamba na maonesho ya bidhaa zinazozalishwa Geita.

Makampuni yaliyodhamini ni GGM, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Maelezo Tv, TADB Bank, NBC na Busolwa Mining Limited.

Wengine ni Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Hifadhi ya Jamii (SSRA), Benki ya Azania, Lenny Hotel, Waja General Company Ltd, GF Truck, Air Tanzania Corporation Ltd, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA).

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu ...

foto
Mwandishi: Hamisi Kibari, Geita

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi