loader
Picha

Dada wa Magufuli kuzikwa leo

WAKATI dada wa Rais John Magufuli, Monica Magufuli anatarajiwa kuzikwa leo, Umoja wa viongozi wa dini nchini umetoa pole kwa Rais Magufuli kutokana na kifo hicho kilichotokea juzi.

Taarifa kutoka Geita zinasema marehemu anatarajiwa kuzikwa leo kijijini kwao Chato mkoani Geita, maziko ambayo yanatarajiwa kuwashirikisha wageni mbalimbali.

Monica ambaye alikutwa na umauti kutokana na ugonjwa wa moyo alikuwa akitibiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza.

Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani, Haki za Binadamu kwa Madhehebu ya Dini nchini, Askofu William Mwamalanga amesema,  kamati hiyo imeguswa na msiba huo kwa kiasi kikubwa.

Askofu Mwamalanga kwa niaba ya Kamati hiyo alimwombea kwa Mungu Rais Magufuli na ndugu wote kuwa na moyo wa uvumilivu na kuitakia pole familia nzima ya Magufuli katika kipindi hiki.

"Sisi Maaskofu na Mashehe 14,860 wa Kamati hii na viongozi wengine wote wa dini tumeguswa na msiba huu uliompata Rais Magufuli"amesema.

Monica ameacha watoto tisa na wajukuu 25.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi