loader
Picha

Vinasaba vyapunguza uchakachuaji mafuta 74%

PROGRAMU ya kuweka vinasaba kwenye mafuta imepunguza uchakachuaji kutoka asilimia 78 ya mwaka 2007 hadi kufikia pungufu ya asilimia nne kufikia mwisho wa mwaka 2017.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Profesa Jamidu Katima ameyasema hayo alipokuwa akilezea mambo ambayo mamlaka hiyo imetekeleza kwa mafanikio kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma iliyokuwa chini ya mwenyekiti wake Dk Raphael Chegeni.

Amesema programu ya kuweka vinasaba kwenye mafuta yote yanayotumika nchini ilianza Septemba 2010 kwa lengo la kuleta usawa katika ushindani na kuhakikisha ubora wa mafuta.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Aprili mwaka 2014 kuhusiana na uwekezaji wa vinasaba katika mafuta kwa lengo la kudhibiti kuuzwa katika soko la ndani mafuta yanayotakiwa kusafirshwa kwenda nchi za jirani umechangia ongezeko la mapato ya kodi kwa kiasi cha Sh bilioni 468.50 kati ya mwaka 2010 hadi mwaka 2013.

Kuhusu Udhibiti wa Bei za Mafuta ulioanza Januari 2009, Profesa Katima alisema bei za mafuta zimefanya Mtanzania kuokoa hadi asilimia 30 kwenye fedha ambazo angetumia kwenye mafuta.

Utafiti wa UDSM uliainisha kuwa udhibiti wa bei za mafuta ulifanikisha kukua kwa pato la ziada kwa kiasi cha Sh bilioni 445.5 kati ya mwaka 2009 na 2010 na hivyo kuongeza mapato ya kodi kwa kiasi cha Sh bilioni 49.

"Pia kutokana na juhudi za EWURA kudhibiti bei za mafuta, kushuka kwa bei ya mafuta katika miezi ya Agosti 2015 na Septemba 2015, kumewezesha kuwapatia watumiaji unafuu katika matumizi ya mafuta kwa kiasi cha Sh bilioni 48.16 na hivyo kutoa fursa ya fedha hizo kuweza kutumia katika shughuli nyingine za kiuchumi."

Kuhusu Mfumo wa Uagizaji wa Pamoja wa Mafuta(BPS), Profesa Katima amesema tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012, mfumo huo umesaidia uhakika wa upatikanaji wa mafuta hapa nchini, kupunguza kwa siku za uchelewesahji wa meli katika bandari ya Dar es Salaam kutoka zaidi ya siku 40 za hapo awali hadi kufikia wastani wa siku 2.

"Pia gharama za uzalishaji na gharama za muuzaji zimekuwa zikishuka tangu kanzishwa kwa mfumo huu kufikia wastani wa dola za Marekani 43.23 kwa tani moja."

Amesema pia kumekuwapo na upatikanaji wa takwimu sahihi za bei na gharama za mafuta na uagizaji wa mafuta (FOB). Kulingana na utafiti uliofanywa UDSM, mfumo huo uliongeza tija kwenye uchumi wa nchi kwa kiasi cha Sh bilioni 121.6 kwa mwaka 2012 na 2013.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi