loader
Picha

Anaswa akimiliki kiwanda cha gobori, bastola

JESHI la Polisi mkoani hapa linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kinamagi, Kata ya Kigwa wilayani Uyui, Mrisho Juma (44) kwa tuhuma za kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha za kienyeji aina ya gobori. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Emmanuel Nley, Juma alikamatwa Septemba 2, mwaka huu nyumbani kwake akiendelea na utengenezaji wa silaha hizo.

Kamanda Nley alisema kuwa mtuhumiwa alikutwa akiendelea kutengeneza magobori matatu pamoja na bastola moja ikiwa imekamilika. Kwa mujibu wa Kamanda Nley baada ya kumhoji mtuhumiwa alikiri kuwa ndiye mtengenezaji wa silaha hizo na huziuza maeneo mbalimbali mkoani hapa. Kufuatia tukio hilo, Kamanda wa Polisi alitoa wito kwa wananchi ambao wanamiliki silaha bila kufuata utaratibu wajisalimishe kabla hatua kali dhidi yao hajachukuliwa. Wakati huo huo, kamanda huyo alisema kuwa jeshi hilo linaendelea kuwashikilia askari polisi 10 wa Wilaya ya Igunga wakihusishwa na kifo cha Selemani Jumapili waliyekuwa wamemkamata kwa mahojiano.

Nley alisema wataalamu kutoka Makao Makuu wa jeshi hilo wanaendelea na mahojiano na askari hao na uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhusika na tukio hilo. Aliongeza kuwa mwili wa marehemu Jumapili ulifanyiwa uchunguzi na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora na taarifa ya matokeo itatolewa mahakamani. Alisema Jumapili alikamatwa na Polisi hao waliokuwa katika msako Agosti 29, saa nane mchana na baadaye akiwa katika Kituo cha Polisi alionekana kuwa mgonjwa na kukimbizwa hospitali na ilipofika saa tano usiku alifariki dunia wakati akipata matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Igunga alipokuwa akipata matibabu.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Tabora

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi