loader
Picha

Nauli Dreamliner kwenda Mumbai yatangazwa

IKIWA imebaki miezi miwili Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kuzindua safari za ndege ya moja kwa moja Mumbai, India kutoka Dar es Salaam, nauli ya safari imetolewa na tiketi zitauzwa mwishoni mwa mwezi huu. Tangazo la nauli hizo kwa vyombo vya habari lilisema jana, safari moja nauli itakuwa Dola za Marekani 286 ikijumuisha na kodi huku nauli kwenda na kurudi ikiwa Dola za Marekani 455. Nauli hiyo ni nafuu ukilinganisha na za ndege za mashirika mengine yanayofanya safari zake kwenda mjini humo ambazo pia haziendi moja kwa moja bali hulazimika kupitia nchi nyingine.

Akizungumza na Habari Leo jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema wametangaza bei hiyo ambayo itakuwa ya kuanzia na promosheni kwa muda. Alisema wamefanya hivyo kuitangaza ndege hiyo, Boeing 787-8 Dreamliner inayobeba abiria 262. “ Nauli za kuanzia ni Dola za Marekani 286 kwenda au kurudi pekee. Safari ya kwenda na kurudi ni Dola 4 55 za Marekani,” alisema. Kagirwa alisema mwisho wa mwezi huu wataanza kuuza tiketi hizo.

Alisema ndege hiyo ya Dreamliner itakuwa ikifanya safari hizo mara tatu kwa wiki na maandalizi yake yamekamilika kwa asilimia 85 hadi 90 sasa na robo mwaka ya mwisho mwaka huu safari hizo zitaanza rasmi. Akieleza kwa nini wameanza safari Mumbai, India, Kagirwa alisema wameangalia uhitaji wa soko ambalo utafiti waliofanya umeonesha una wateja wengi wa kwenda moja kwa moja huko. Alitaja sababu nyingine ni uhusiano wa India na Tanzania wa muda mrefu na fursa za biashara nyingi na wanaoenda kwa matibabu na elimu.

Kagirwa alisema wateja wa nchi za Afrika Mashariki wamesogezewa usafiri kwenda India kwa kuzindua safari za E ntebe na Bujumbura wanakoweza kuunganisha ndege ya Mumbai. Alisema safari za nje E ntebbe na Bujumbura ni maandalizi mazuri ya kwenda miji mingine ambapo sasa kinachosubiriwa ni kuwasili kwa ndege mpya mbili aina ya Airbus A220-30 0 . Alisema ndege hizo zilizotengenezwa Canada zitawasili Novemba mwaka huu na kuongeza idadi ya ndege zitakazofanya safari ndani na nje. Alisema Dreamliner itamaliza ratiba ya safari za ndani mwisho wa mwezi huu kujiandaa kwenda Mumbai na ndege Airbus A220-30 0 zikiwasili, zitaongeza nguvu kwa safari za masafa marefu kwenda China, Thailand na nchi nyingine nje.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi