loader
Picha

‘Ni zamu ya Kenya Afcon’

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Michael Olunga anaamini kuwa wakati umefi ka kwa Kenya kurejea katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon). Olunga aliiongoza Harambee Stars kuvisambaratisha vigogo vya soka Afrika, Ghana baada ya kuwafunga 1-0 katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za mwaka 2019 katika mchezo wa Kundi F uliofanyika kwenye Uwanja wa Kasarani mwishoni mwa wiki iliyopita. Kenya walipata bao hilo baada ya beki wa Ghana, Nicholas Opoku kuujaza mpira kwenye lango lao wakati akijaribu kuokoa mpira wa krosi kutoka kwa Eric Johanna.

Kwa ushindi huo, Kenya sasa wana pointi sawa na Ghana baada ya kucheza raundi mbili kabla ya mchezo dhidi ya Ethiopia utakaofanyika Oktoba 10 ama 13. “Naamini wakati umefika kwetu (kurejea katika fainali za Afcon) baada ya miaka kibao ya kuwa nje ya mashindano hayo. Binafsi inabidi kufanya kazi kwa bidii na kujaribu kuwafurahisha mashabiki wa nyumbani kila ninapopata nafasi,” alisema.

Mshambuliaji huyo anayecheza soka Japan aliongeza: “Ni heshima kubwa kuchezea timu ya taifa na tunatarajia kutakuwa na ushawishi mkubwa… tuna mechi mbili zaidi nyumbani mbele ya mashabiki wetu kama ile tuliyocheza juzi dhidi ya Ghana. Tunaweza kupata pointi tatu na kufuzu.” Mchezaji huyo wa zamani wa Gor Mahia, pia alilishukuru Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kwa kuwaunga mkono, huku akitoa changamoto kwa Serikali kupitia Wizara ya Michezo, kuwasilisha bajeti ya timu mapema.

“Tunaridhika na kile kilichofanywa na FKF hadi sasa na pia tunaishukuru serikali kwa kutoa tiketi mapema…. “Pia wanatakiwa kuimarisha miundo mbinu nchini ili kupiga jeki soka la hapa nchini, na tunatakiwa kuwa na shule nyingi za soka, na viwanja vingi na vizuri vya kuchezea kama vile Kasarani, ambacho bila shaka wataendelea kuutunza vizuri,” alikamilisha mchezaji huyo.

KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi