loader
Picha

Mwanafunzi adaiwa kumuua ndugu kwa panga

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Iringa, Suguta Mniko amedaiwa kuuawa na kaka yake, Wegesa Mniko maarufu kwa jina la Ostas baada ya kumkata kwa mapanga kichwani na mguuni. Tukio hilo lilitokea juzi wakati Suguta alipoingia nyumbani kwa kaka yake huyo, wote wakiwa wadogo zake Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema), saa nane usiku, akitokea kwenye mkesha wa mbio za Mwenge.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe alithibitisha kutokea tukio hilo na kubainisha kuwa baada ya mwanafunzi huyo kuingia ndani, kaka yake (Ostas) aliyekuwa amelewa pombe alimparamia na kuanza kumkata mapanga akidhania kuwa ni vibaka wanaingia kwake. Alisema Ostas alimkatakata mdogo wake kichwani na miguuni na baadaye alikimbia. “Jeshi la Polisi linamsaka mtuhumiwa Wegesa (Ostas) kwa mauaji ya mdogo wake, Suguta.

Aliwataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi na kutochukua uamuzi wa kuwakata watu wengine na kusababisha madhara na vifo visivyo na msingi,” alisema Kamanda huyo. Alisema Wegesa amesababisha kifo cha mdogo wake aliyeacha pengo kubwa kwa familia yake kwani alikuwa tegemeo la taifa na familia yao. Alisema mwili wa Suguta upo chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa uchunguzi zaidi. “Tunaomba wananchi kutoa taarifa kwa Polisi mtuhumiwa atakapoonekana au kujisalimisha Polisi kabla ya kukamatwa,” alisema Kamanda.

TANZANIA na Uganda zimeanzisha rasmi Jukwaa la Biashara baina ya ...

foto
Mwandishi: Samson Chacha, Tarime

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi