loader
Picha

10% wajisaidia porini Chamwino

WILAY A ya Chamwino mkoani Dodoma ina asilimia 34 tu ya kaya zenye vyoo bora na asilimia 10 ya watu wanaojisaidia hovyo. Hayo yalibainika juzi wakati wa uzinduzi wa mkakati wa ujenzi wa vyoo bora, ulioasisiwa na Diwani wa Buigiri, Keneth Y indi, ambapo benki ya Equ ity itawezesha mikopo ya vikundi kwa ajili ya ujenzi wa vyoo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mkakati huo, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Steven Kibirti alisema wilaya ya Chamwino inashika nafasi ya 124 katika halmashauri zote ambapo ina asilimia 34 ya nyumba zenye vyoo bora. Hata hivyo, alibainisha kuwa katika wilaya hiyo, kuna asilimia 10 ya watu wanaojisaidia ovyo. Kibiriti alisema wana imani kubwa kuwa kampeni ya ujenzi wa vyoo bora vya aina ya sato utasaidia kuongezeka kwa wenye vyoo bora hadi kufikia asilimia 100.

Alisema ujenzi wa vyoo kwa muda mrefu umekuwa hauzingatii viwango vya ujenzi hali ambayo imekuwa ikisababisha vyoo vingi kubomoka wakati wa mvua. “Unaweza kujiuliza kwa nini choo kinabomoka lakini nyumba hazibomoki lakini ukiangalia utaona. Nyumba zina paa lakini vyoo haviezekwi, hali inayosababisha kuta zake kulowana na kujaa maji wakati wa mvua na mwishowe kubomoka. Mnatakiwa kuezeka vyoo ili maji yadondokee pembeni ya kuta ili vyoo visibomoke,” alisisitiza.

Ofisa Afya wilaya ya Chamwino, Cuthbert Kongola alisema wakati wa kampeni ya ujenzi wa vyoo bora iliyozinduliwa mwaka 2012 na R ais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete na wakati huo kaya zenye vyoo bora zilikuwa chache. Alisema mwaka 2017 baada ya kujipanga, walipanda na kufikia asilimia 98 ya kaya zenye vyoo ambapo asilimia 47 ya kaya zilikuwa na vyoo vilivyoboreshwa. Alisema sasa kaya zenye vyoo ni asilimia 91, kaya zisizo na vyoo ni asilimia tisa na vyoo vilivyo bora asilimia 37.

Alisema mwaka 2017 walishika nafasi ya kwanza kiwilaya kwani kila kaya ilikuwa na choo. Kongola alisema Julai mwaka huu hali ya vyoo ilikuwa mbaya kwani kaya 270 zilikuwa hazina vyoo baada ya vyoo kubomoka kutokana na mvua na kuongeza kuwa mpaka sasa ujenzi kwa ajili ya vyoo vilivyobomoka unaendelea vizuri. Meneja uendeshaji Biashara wa kampuni inayouza vyoo vya Sato vinavyouzwa kwa Sh 11,000, Avit Buchwa alisema vyoo hivyo ni rahisi kusafishika, vinazuia wadudu na harufu na mtoto anaweza kuingia na kujisaidia bila wasiwasi.

Diwani wa kata hiyo, Y indi alisema Buigiri ni makao makuu ya wilaya ya Chamwino na mkakati uliopo ni kuhakikisha kila nyumba inakuwa na choo bora. Ofisa Afya kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu Dodoma, R ichard L upeja alisema kulikuwa na changamoto ya kuboresha vyoo. Meneja wa benki ya Equity, Upendo Makila alisema benki itakopesha wananchi walio kwenye vikundi ili wajenge vyoo bora. Mdau wa maendeleo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Dk. Ombeni Msuya alisema vyoo bora ni muhimu kwa ustawi wa afya za wananchi.

TANZANIA na Uganda zimeanzisha rasmi Jukwaa la Biashara baina ya ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Chamwino

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi