loader
Picha

Kifua kikuu chaua watu 27,000

WATU 154,000 huugua kifua kikuu (TB) na kati yao 27,000 hufariki dunia ambao ni sawa na vifo 74 kwa siku. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alisema vifo vinavyotokana na TB vilishuka kutoka watu 58 kwa kila watu 100,000 mwaka 2014 hadi watu 47 kila watu 100,000 kwa mwaka.

Dk Ndugulile alitoa kauli hiyo wakati akizundua rasmi TB-Caucus ya wabunge, ambao ni mtandao wa wabunge wa mapambano dhidi ya kifua kikuu. Alisema serikali imeweka msukumo wa kupima ugonjwa huo kutokana na kufunga mashine 209 za kisasa za kupima, ambazo mgonjwa hahitaji kwenda mara tatu kuchukua majibu, badala yake atachukua majibu ndani ya saa mbili. Alisema serikali imweka msisitizo ndio maana inatoa dawa bure na matibabu bure kwa wagonjwa wanagundulika kwamba wanasumbuliwa na TB.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stella Ikupa alisema ugonjwa huo unawakumba familia maskini, hivyo ni wajibu wa wabunge kwenda kuelimisha jamii kuhusu kupima na kujua afya zao kuhusu ugonjwa huo. Meneja wa Kifua Kikuu Tanzania, Dk Beatrice Mtayoba aliwaomba wabunge watumie nafasi zao kuhamasisha jamii kwenda kupima kifua kikuu. Aliwataka wabunge watumie utashi wa kisiasa katika kuongoza mapambano dhidi ya kifua kikuu na waiweke ajenda ya kuhamasisha watu kupima mipango yao ya kila siku. Pia wanatakiwa kuhamasisha serikali iweke kipaumbele na kuongeza bajeti katika kupambana na maradhi hayo, ambayo yanaua zaidi kuliko maradhi mengine.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi