loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkazi wa Babayu ajinyonga shambani

MKAZI wa Kijiji cha Babayu Msangani Wilaya ya Bahi, Mohamed Y ahaya Mduli (50), amekutwa amejinyonga shambani kwake na kuacha ujumbe akazikwe nyumbani kwa mama yake. Tukio hilo limethibitishwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Jumanne Mohamed Seleman. Alisema mwili wa Mohamed ulikutwa juzi unaning’inia katika tawi la mti shambani kwake majira ya saa 3 asubuhi.

“Inasikitisha sana ,marehemu ameacha ujumbe kuwa azikwe nyumbani kwa mama yake mzazi lakini sababu za tukio hili bado hazijajulikana wala hakuziandika,” alisema. Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi kuacha kuchukua maamuzi ya namna hiyo na kama wana msongo wa mawazo, watafute njia sahihi ya kutatua matatizo yanayowakabili . “Kuna watu wameathirika kisaikolojia kutokana na sababu mbalimbali, niwaombe watanzania wenzangu tusijiuzulu tutafute njia mbadala hata kwa wataalamu wa saikolojia,” alisema. Shuhuda wa tukio hilo, ambae ni kaka wa marehemu, Sumbwi Mduli alielezea masikitiko yake na namna lilivyotokea.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Bahi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi