loader
Picha

Ndugai kuzindua Miss Journalism World 2018 leo

UZINDUZI wa shindano la Miss Journalism World 2018 unatarajiwa kufanyika leo mjini hapa ambapo Spika wa Bunge, Job Ndugai anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu katika Hoteli ya Ngurdoto Arusha na kushirikisha washiriki kutoka nchi zaidi ya 60. Mratibu wa Miss Journalism World, Samwel Chazi, alithibitisha Ndugai kushiriki kwenye uzinduzi huo unaofanyika kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Mbali na Ndugai katika hafla hii, tumewaalika viongozi wa Kamati 15 za Bunge, mawaziri, mkuu wa mkoa wa Dodoma na waheshimiwa wabunge,” alisema. Chazi alisema, shindano hilo linatoa fursa kwa nchi kutangaza vivutio vya utalii kimataifa hasa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Bonde la Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro na Olduvai G eorge.

“Aidha pia shindano hili litatoa fursa kwa nchi kutangaza utalii wa kitamaduni,” alisema. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Journalism World, Philemon Mollel alisema shindano hilo la urembo lilibuniwa kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika, lakini lengo kubwa ni kuitangaza zaidi Tanzania. “Naomba wadhamini wanaotaka kujitokeza kudhamini wafanye hivyo, kwani tunahitaji sana sapoti yao,” alisema. Uzinduzi wa leo wa tiketi za kidiplomasia utakaofanywa na Spika Ndugai utasindikizwa na bendi ya Mjengoni Classic kutoka Arusha.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi