loader
Picha

Samia ataka Kigoma wasifiche wahamiaji

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametaka wakazi wa vijiji vya mwambao wa Kusini wa Ziwa Tanganyika wasikumbatie na kuwahifadhi wahamiaji kutoka nchi za ukanda wa maziwa makuu kujilinda na ugonjwa wa Ebola. Mama Samia alitoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwakizega wilaya ya Uvinza akiwa katika ziara ya kiserikali ya siku nne mkoani Kigoma.

Alisema sasa ugonjwa huo upo nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari. Alisema ugonjwa huo haujaingia nchini lakini DRC ni jirani na mkoa Kigoma hivyo kuhifadhi wageni hawajapitia njia rasmi za kuingia nchini kunachangia kuingiza maambukizi hayo nchini. Katika hatua nyingine, Mama Samia amesema serikali imejizatiti na kuuangalia mkoa Kigoma kama mkoa maalum wa kimkakati kiuchumi.

Alisema ziara za viongozi wa kiserikali akiwemo Rais John Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ni kutekeleza mpango wa kuufanya mkoa huo kutekeleza mipango hiyo. Alisema ni lazima wananchi wa mkoa Kigoma wakae mkao wa kula kutekeleza mipango ya maendeleo na kiuchumi inayoletwa na serikali. Akizungumzia ujenzi wa kituo cha afya Uvinza alisema mradi huo ni maboresho makubwa yanayofanywa na serikali katika sekta ya afya nchi nzima ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa madawa muhimu kwa wananchi wakati wote. Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza, Weja Ngolo alisema shilingi milioni 400 kimetolewa kwa ujenzi wa kituo cha afya Uvinza ambapo shilingi milioni 367 zimeshatumika na ujenzi umekaribia kuisha.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Fadhili Aballah, Kigoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi