loader
Picha

Madiwani TLP, Chadema wahamia CCM

MADIWANI wawili mmoja akiwa ni wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mwingine wa Tanzania Labour P arty (TLP ), katika Halmasauri ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, wamevihama vyama vyao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Madiwani hao wamebainisha kuwa wameamua kuhama vyama vyao baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli, hivyo haipo sababu ya kuendelea kuwa katika vyama vyao. Madiwani hao ni pamoja na Alex Paul Musege wa kata ya Kasuguti kupitia tiketi ya Chadema na Abiud Mugesi Chacha, wa kata ya Butimba, kupitia tiketi ya TLP, ambao wote kwa pamoja jana, mbele ya viongozi wa CCM wilayani hapa walitangaza rasmi kuvihama vyama vyao na kujiunga na CCM.

V iongozi wa CCM wilayani Bunda waliowapokea madiwani hao baada ya kutangaza kuvihama vyama vyao ni pamoja na mwenyekiti wa CCM wa Wilaya, Justine Rukaka, katibu Mabutu Malima na katibu wa siasa na uenezi, Jasper Bonaventre. Alisema Rais Magufuli anafanyakazi nzuri inayopaswa kuungwa mkono na wananchi wote na kutoa wito kwa kwa wanachama wengine ambao bado wako kwenye vyama vya upinzani kuhamia CCM. Chacha alisema kuwa amekihama chama chake kwa hiari yake mwenyewe na kwamba hatua hiyo ni kutokana na kurizika na utendaji kazi wa Rais Magufuli.

Alisema kiongozi huyo amekuwa mstari wa mbele kuwaletea wananchi maendeleo, ikiwemo kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo. Alisema kuwa Rais Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuletea wananchi maendeleo tena kwa kutumia fedha za ndani, jambo ambalo limemfanya achukuwe uamuzi huo. Kwa upande wake, Katibu wa CCM wilayani Bunda, Mabutu Malima, alisema kuwa wameamua kuwapokea wanachama hao wapya kwa heshima kubwa kwani ni watoto waliokuwa wamepotea na sasa wameamua kurudi nyumbani. Malima aliongeza kuwa kama kuna wanachama wengine wa vyama vya upinzani wanaotaka kujiunga na chama hicho wanakaribishwa kwani CCM ni chama makini na chenye mlengo wa kuletea wananchi maendeleo na ni tofauti kabisa na vyama vingine vya upinzani.

Alisema kuwa hakuna ubishi kwamba Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, tangu alipoingia madarakani anafanya kazi nzuri na pia chama hicho kiko kwenye misingi imara. Aidha, alisema hakuna ubishi kuwa Rais Magufuli anaendelea na jitihada zake za kuhakikisha hawatokei wabadhirifu wa mali za umma na kuongeza kuwa kwa msingi huo ndiyo maana wananchama wa vyama vingine kila kukicha wanaamua kujiunga na CCM kwa kasi kubwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Amos Kusaja, jana alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa safarini, alisema kuwa alipigiwa simu na diwani mmoja kati ya hao wawili alithibitisha kwamba tayari wameshapeleka barua zao katika ofisi yake ya kuhama vyama vyao na kuachia nafasi ya udiwani.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Ahmed Makongo, Bunda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi