loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makonda atoa mwezi barabara kukamilishwa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam P aul Makonda ametoa mwezi mmoja kwa Kampuni ya ujenzi wa barabara ya Nyanza kukamilisha ujenzi wa barabara inayojengwa kupitia mradi wa Uendelezaji Miundombinu ya jiji la Dar es Salaam (DMDP) katika eneo la Chang’ombe, wakishindwa Manispaa ya Temeke ivunje mkataba. Mbali na kutoa mwezi mmoja, Makonda pia ameitaka kampuni hiyo kuvunja na kujenga upya mitaro waliyojenga katika barabara ya Mchicha hadi Temeke Maghorofani yenye urefu wa kilomita 1.8, kwa kuwa mitaro iliyojengwa haiendani na ubora uliotakiwa.

 

Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 1.9 ilipaswa kukamilika ndani ya miezi 15 lakini mpaka sasa mkandarasi ametumia miezi 11 bila kufikia nusu ya ujenzi huo licha ya kuwa wameshalipwa fedha. Makonda alitoa maagizo hayo jana wakati alipotembelea barabara zinazojengwa katika Manispaa ya Temeke chini ya DMDP na Wakala wa Barabara za V ijijini na Mijini (TARURA). “Nakuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi mfatilie huyu Mkandarasi wa Nyanza ndani ya mwezi mmoja awe amekamilisha ujenzi wa barabara tulizomkabidhi, akishindwa vunjeni mkataba mtafute mkandarasi ambaye ataweza kufanya kazi kwa kuwa wananchi wanahitaji maendeleo,”alisema.

Makonda alisema endapo mkandarasi huyo atashindwa kukamilisha mradi huo atakuwa amepoteza sifa ya kupewa kazi katika mkoa huo na kuziagiza halmashauri zote kitompa zabuni nyingine mpaka akamilishe ujenzi huo. “Wekeni bidii nataka nione barabara inatumika na mkishindwa hamtopewa kazi nyingine, wapo wakandarasi wenye kasi na uwezo wa kujenga, haiwezekani miezi 11 hakuna kilichofanyika nataka kazi,”aliongeza. Alisema anashindwa kuelewa mkandarasi huyo amekwama wapi licha ya kuwa fedha za mradi huo zipo na kinachotakiwa ni utekelezaji wa wakandarasi waliopewa mradi.

IKIWA fomu moja ya kuomba ridhaa ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi