loader
Picha

Yanga haichomoki - Stand United

STAND United imepania ‘kufa’ n a Y anga katika mechi ya Ligi Kuu itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Jumapili ya wiki hii. Ligi hiyo inaendelea tena baada ya kusimama kwa takribani wiki mbili kuipisha timu ya taifa, Taifa Stars kucheza mechi ya kimataifa dhidi ya Uganda. Kocha msaidizi wa Stand, Athuman Bilal ameahidi kuwafunga mabingwa hao wa zamani na kuwataka wasahau kupata pointi kwao.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu jana, Bilal alisema timu yake imekuwa ikijifua vyema kuelekea mchezo huo. “Baada ya mchezo wetu na Biashara tulikwenda kuweka kambi Biharamulo kujiandaa na Y anga… timu yangu iko vizuri na matokeo mazuri tunatarajia kuyapata,” alisema. Alisema kuelekea mchezo wao na Y anga hakuna majeruhi yoyote na vijana wake wapo tayari kuikabili Y anga. Alisema timu yake inatarajiwa kuondoka Shinyanga kesho kuifuata Y anga Dar es Salaam.

Alisema anatarajia mchezo huo utakuwa mgumu ila wao mikakati yao ni kuhakikisha wanashinda na kupata pointi tatu. Aliwaomba wadau na wapenzi wa soka wa klabu yao kuungana kuisapoti timu hiyo ifanye vizuri. Baada ya mchezo wao na Y anga, Stand United itacheza na timu ya manispaa ya Kinondoni (KMC) kisha itasafiri kuelekea Mtwara kwenda kuikabili Ndanda F C. Katika msimamo wa Ligi Kuu, Stand United ipo katika nafasi ya tano ikiwa na pointi sita baada ya michezo mitatu. Timu hiyo ilishinda mechi mbili kwa bao 1-0 dhidi ya Biashara United na African Lyon. Pia ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa CCM Kambarage.

TANZANIA na Uganda zimeanzisha rasmi Jukwaa la Biashara baina ya ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi