loader
Picha

Simba yaifuata Ndanda kibabe

KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuondoka leo kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nang’wanda keshokutwa. Akizungumza jana, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema wachezaji wanne walioruhusiwa kwenda kuchezea timu zao za taifa kwenye mechi za Kimataifa mwishoni mwa wiki iliyopita, wamerejea isipokuwa kiungo Mzambia Cletus Chama ambaye anatarajiwa kuwasili leo kuungana na wenzake kwa safari ya Mtwara. “

Juuko Murshid, E mmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Meddie Kagere wamerejea na jana jioni (juzi) walifanya mazoezi na wenzao,” alisema Manara. Alisema wachezaji 20 watasafiri kwenda Mtwara kucheza mechi ya kwanza ya ugenini na ya tatu kwa msimu baada ya kushinda mechi za awali nyumbani dhidi ya timu za Mbeya, Tanzania Prisons na Mbeya City. Pia alisema kiungo Muzamil Y assin hatokwenda Mtwara kwa sababu yupo katika mapumziko baada ya kuoa wiki iliyopita kwani pia ni majeruhi.

Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea kuanzia kesho baada ya kupisha mechi za kimataifa na kutachezwa michezo miwili, Mwadui F C ikiikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na African Lyon dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Ligi itaendelea keshokutwa kwa Lipuli wakiikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Samora Iringa, Ndanda na Simba katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Tanzania Prisons na Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine Mbeya Mbao FC na JKT Tanzania Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, KMC na Singida United Uwanja wa Taifa na Biashara United na Kagera Sugar Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Musoma,Mara. Y anga watateremka Uwanja wa Taifa Jumapili kumenyana na Stand United, huo ukiwa mchezo wao wa pili baada ya ushindi wa 2-1 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar.

KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi