loader
Picha

NEMC YACHUNGUZA MAJI YA KEMIKALI MARA

AGIZO lilitolewa na Rais John Magufuli akiwa ziarani mkoani Mara juu ya madai ya kuwepo kwa baadhi ya migodi ya madini inayotiririsha maji yenye kemikali zenye sumu kwenye mito ambayo maji yake yanatumiwa na wananchi kunywa, imeliamsha Baraza la Taifa na Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambalo limechukua sampuli ya maji hayo mara moja ili kuanza uchunguzi wa kina. Ili kufanyia kazi kwa kina agizo hilo la Rais Magufuli, wataalamu kutoka NEMC kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wamechukua sampuli zaidi ya 10 ya maji kutoka katika vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kuona kama maji hayo yana kemikali zenye madhara kwa viumbe hai.

Sampuli ya maji hayo yanayodhaniwa kuwa na kemikali yanayotiririka kutoka katika Mgodi wa Acacia North Mara mpaka kwenye makazi ya watu. Akizungumza wakati kazi hiyo ikiendelea mkoani Mara jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Vedast Makota alisema NEMC imeanza kutekeleza agizo hilo kwa kuchukua sampuli katika maeneo yote ili kubaini kama zina madhara kwa viumbe hai au la. “NEMC kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali watafika kila mahala ikiwemo kupitia vibali vyote vya awali ili kubaini kama utolewaji wa vibali hivyo ulikidhi vigezo vinavyotakiwa na kuona kama wamiliki wa mgodi huo wanazingatia masharti yaliyoagizwa katika vibali hivyo,” Dk Makota alisisitiza.

Alisema utafiti wao utaenda sanjari ya uchukuaji sampuli mbalimbali yakiwemo maji, mimea na mchanga ambapo watahakikisha wanashirikiana na jamii inayozunguka mgodi huo ili kufanikisha kazi nzima kuona kama kuna viashiria vinavyoshukiwa kuwa na chembe chembe zenye kemikali. “Tupo katika hatua za awali za utekelezaji wa agizo hilo ambapo wataalamu wametembelea maeneo ya Mto Tighite, ambao kwa kiasi kikubwa maji yake ndiyo yanatumika sana wakazi wa eneo hilo kwa shughuli mbalimbali za kijamii,” alisema.

KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mara

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi