loader
Picha

TAA yakanusha madai wizi JNIA

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imemtaka mwanamama Awateef Akrabi aliyedai kuibiwa pochi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuomba msamaha. Hiyo ni baada ya teknolojia uwanjani hapo kubaini kuwa mwanamama huyo alidanganya kuhusu taarifa hiyo aliyoisambaza kwenye mitandao ya kijamii. Mwanamama huyo aliandika taarifa ambayo inazidi kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii akilalamikia kuibiwa pochi yake baada ya kukaguliwa kwenye sehemu ya mwisho ya ukaguzi wa abiria ya uwanjani hapo.

Katika malalamiko yake mwanadada huyo alisema licha ya kulalamikia wizi huo kwa wakaguzi wa eneo husika hakusikilizwa na alipuuzwa huku akielezea kuwa alikataliwa kuangalia picha za ukaguzi zilizorekodiwa kwa njia ya CCTV kamera. Akizungumzia sakata hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela alibainisha kuwa baada ya kuuona ujumbe huo wa malalamiko kwenye mitandao, ofisi yake ikishirikiana na wataalamu wa uchunguzi uwanjani hapo waliamua kufuatilia kwa undani zaidi.

Alisema, askari pamoja na wataalamu wengine walianza kwa kufuatilia kamera hizo za CCTV ili kubainisha wizi unaodaiwa kufanyika ambapo kamera hizo zilimuonesha akigaguliwa kuanza sehemu ya kwanza hadi mwisho lakini hakuna sehemu inayoonesha akiibiwa. Alisema, kwa kuwa lawama zilielekezwa zaidi kwenye sehemu ya mwisho ya ukaguzi wataalamu wa uchunguzi wa JNIA walitumia muda mwingi zaidi kuzifuatilia kamera kwenye sehemu hiyo ili kubainisha kama aliibiwa lakini hakukuwa na ushahidi huo.

Kwenye mkutano huo wa wandishi wa habari uliohudhuriwa pia na ndugu wa mama huyo, ilioneshwa video hiyo nzima ambapo kaka wa mwanamama huyo, Wael Akrabt, aliyesema dada yake hakuibiwa uwanjani huku akibainisha kuwa tangia juzi waliitwa uwanjani hapo kuangalia video hizo. Kwa mujibu wa Mayongela, mama huyo aliondoka nchini Septemba 8, kuelekea nchi za Ghuba akiwa na watoto wawili, ambapo mbali na kudai kuibiwa pochi pia alitoa tuhuma nyingi kama vile kuzimwa kwa mashine za ukaguzi, kunyang’anywa maji ya kunywa ya watoto wake, kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wakati wa ukaguzi hali iliyochangia kuibiwa kwa pochi hiyo.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi