loader
Picha

Ubora waongeza shehena bandari ya Kigoma

MABORESHO makubwa yanayoendelea kufanywa katika bandari ya Kigoma yameiwezesha bandari hiyo kujiendesha kwa ufanisi kwa kuongeza shehena na kujiendesha bila kutegemea ruzuku. Kutokana na mafanikio hayo bandari hiyo imeongeza ukusanyaji mapato kutoka Sh bilioni 4.1 mwaka 2016/17 hadi kufikia Sh bilioni 6.8 mwaka 2017/18. Meneja wa bandari za ziwa Tanganyika, Ajuaye Kheri Msese alisema hayo wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa mkoa Kigoma, Emanuel Maganga aliyeongoza kamati ya ulinzi kutembelea bandari ya Kigoma na kuzungumza na wadau wanaofanya shughuli zao kutumia bandari hiyo.

Msese alisema kuwa kwa mwaka 2017/18 shehena ya mzigo unaopitia bandari hiyo kwenda Zambia na nchi za Maziwa Makuu iliongezeka na kufikia tani 196,000 ukilinganisha na shehena iliyopitishwa bandarini hapo mwaka 2016/17 ambapo tani 136,000 ndiyo zilisafirishwa. Alisema kuongezeka kwa shehena kumeenda sambamba na kuongezeka kwa mapato hivyo kuifanya bandari hiyo kujiendesha kwa kujitegemea badala ya kutegemea ruzuku ambapo kwa sasa bandari ya Kigoma inashika nafasi ya pili kwa kuingizia nchi mapato na kuwa na idadi kubwa ya shehena inazosafirisha.

Hata hivyo, alisema kuwa bado upatikanaji wa mabehewa machache unakwaza mpango wa bandari kuongeza usafirishaji wa shehena na kuongeza mapato na kwamba upatikanaji wa mabehewa mengi na kwa wakati kunasaidia kuvutia wasafirishaji wa shehena wa nchi za maziwa makuu kutumia bandari ya Kigoma.

Akieleza mipango mingine inayofanyika mkoani humo ni pamoja na ujenzi wa bandari kavu ambayo itakuwa chachu ya ongezeko kubwa la shehena na kwa muda mfupi kwani wasafirishaji wataweza kuchukua shehena zao kutokea Kigoma badala ya kwenda Dar es Salaam. Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa mkoa Kigoma, Maganga alisema serikali inatekeleza mkakati wa kuweka mazingira mazuri ya kiuchumi kwa watu wake na kuboreshwa kwa bandari. Alisema kuwa bandari ya Kigoma inao mchango mkubwa wa mafanikio ya bandari ya Dar es Salaam na nchi kwa jumla kwani kwa sasa inapokea shehena zinazokwenda nchi za maziwa makuu hivyo kupoteza soko hilo kutaifanya nchi kupoteza mapato.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi