loader
Picha

Ni wakati wetu -Yanga

YANGA imesema, kucheza mechi nyingi Dar es Salaam ni nafasi yao kupambana kulirejesha taji la Ligi Kuu Bara linaloshikiliwa na watani wao wa jadi, Simba. Ratiba inaonesha Yanga itacheza mechi 11 Dar es Salaam ambapo saba itakuwa nyumbani na nne ugenini. Pamoja na kuonekana itakuwa ugenini kwenye baadhi ya mechi, lakini uwanja wa Taifa Dar es Salaam umezoeleka na timu hiyo na hivyo itakuwa kama iko nyumbani.

Tangu juzi kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na maneno ya hapa na pale kutoka kwa wadau wa soka kuhusu ratiba hiyo kwa upande wa Yanga kwamba inacheza mechi nyingi nyumbani, jambo ambalo si kweli. Keshokutwa, Yanga itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Taifa, ikiwa ni mechi yake ya pili ya Ligi Kuu msimu huu, baada ya kuifunga Mtibwa Sugara mabao 2-1 katika mechi ya kwanza.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika, alisema uongozi wameipokea vizuri ratiba hiyo na watapambana kuhakikisha wanapata pointi zote. “Si fursa bali ni mapambano kama fainali kwa kila mechi maana kuna faida na hasara zake unapopata ratiba kama hii,” alisema Nyika. Michezo hiyo ni Yanga dhidi ya Stand Utd, Yanga dhidi ya Coastal Union, Yanga dhidi ya Singida Utd, JKT Tanzania dhidi ya Yanga, Simba dhidi ya Yanga, Yanga dhidi ya Mbao FC, Yanga dhidi ya Alliance FC. Mechi zingine ni KMC dhidi ya Yanga, Yanga dhidi ya Lipuli FC, Yanga na Ndanda FC na African Lyon na Yanga.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi