loader
Picha

Azam ishindwe yenyewe leo

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi mbili baada ya kusimama kwa karibu wiki mbili kupisha mechi za kimataifa za kufuzu fainali za Mataifa Afrika (Afcon 2019). Mabingwa wa Kombe la Kagame, Azam FC watakuwa kwenye uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga kucheza na wenyeji wao Mwadui FC na Coastal Union itawafuata African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Huu ni mchezo wa tatu kwa Azam iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi mbili dhidi ya Mbeya City na Ndanda FC.

Mwadui wanashika nafasi ya pili kutoka mkiani mwa msimamo, wamecheza michezo miwili ambayo yote wamefungwa. Kama Azam itaondoka na pointi angalau moja itampokonya Mbao usukani wa ligi, watakuwa sawa kwa pointi saba lakini Azam ina uwiano mzuri wa mabao, Mbao wanatarajiwa kucheza na JKT Tanzania kesho. Mchezo wa African Lyon na Coastal unatarajiwa kuwa mkali kutokana na timu hizi ni kati ya sita zilizopanda Ligi Kuu msimu huu hivyo kila mmoja anahitaji kuziona.

Coastal baada ya kucheza mechi tatu imeshinda moja na sare mbili imejikita nafasi ya sita, huku African Lyon inayonolewa na Mfaransa, Soccola Lionel, inashika nafasi ya 16 ikiwa imecheza mechi tatu, imetoka sare mbili na kufungwa moja. Akizungumzia mchezo huo, meneja wa Azam FC, Philip Alando alisema kuwa siku zote mechi za ugenini huwa ngumu lakini kutokana na maandalizi waliyoyafanya wanaamini hawatatoka patupu.

Aliongeza kuwa katika mchezo huo kuna hatihati ya kumkosa kiungo wao, Tafadzwa Kutinyo ambaye amechelewa kujiunga na wenzake baada ya kuwa kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya Zimbabwe. “Kikosi kipo kamili kwa mchezo huo, wote wapo kasoro Kutinyo ambaye atajiunga na timu kesho (leo), amechelewa alikuwa na timu yake ya taifa, sijajua kama kocha atamtumia au la inategemea na mahitaji yake.

KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi