loader
Picha

Faini kwa kahaba Sh500/-, atashindwaje kulipa? Masauni ahoji

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imelieleza Bunge kuwa, kiwango kidogo cha faini wanazotozwa wenye madanguro kimekuwa kikwazo katika mapambano dhidi ya biashara ya ukahaba. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Alhaj Hamad Yusuph Masauni amesema jijini Dodoma kuwa, ukahaba unahusisha makundi mbalimbali wakiwemo wanawake wanaojiuza, wanaume wanaonunua na wenye madanguro. Wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Zainabu Vullu, Mhandisi Masauni amesema, kuna haja ya Bunge kuzitatua changamoto zinazohusiana na biashara hiyo ikiwemo sheria iliyopitwa na wakati. "Ukiangalia kwenye Kanuni za Adhabu Namba 176A Sura ya 16 adhabu ambayo inatakiwa itolewe kwa watu ambao wanafanya biashara ya madanguro wanasema ni faini isiyozidi shilingi 500 na iwapo ni kosa la mara ya pili na kuendelea ni faini isiyozidi shilingi 1,000"amesema. Amewaeleza wabunge kuwa, adhabu kama hiyo inaweza kuhamasisha kuendelea kwa ukahaba hivyo kuna haja Bunge lizipitie sheria zilizopitwa na wakati ili kazi ya kukamata makahaba na wengine wanaoshiriki kwenye biashara hiyo iwe na tija. Wakati anajibu swali na msingi la Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia, Masauni amesema, ukahaba ni suala mtambuka hivyo ili kuukabili unahitajika ushirikiano wa wadau wengi zikiwemo Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Katiba na Sheria, na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,

TANZANIA na Uganda zimeanzisha rasmi Jukwaa la Biashara baina ya ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi