loader
Picha

Wizara: Mishahara haichelewi zaidi ya tarehe 24

Wizara ya Fedha na Mipango imelieleza Bunge kuwa, hakuna ucheleweshaji wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma.
Naibu waziri wa Wizara hiyo, Dk. Ashatu Kijaji, amesema bungeni jijini Dodoma kuwa, kwa mujibu wa Waraka wa Hazina Namba 12 wa mwaka 2004, watumishi wa umma wanatakiwa kulipwa mishahara yao kabla ya tarehe 25 ya kila mwezi.

Ameyasema hayo wakati anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mwantum Dau Haji. Mbunge huyo alitaka kufahamu lini Serikali itamaliza tatizo la kuchelewa mishahara ya watumishi wa umma.

"Kumbukumbu za malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma zinaonesha kuwa, kuanzia Julai 2017 hadi Agosti 2018 watumishi walilipwa mishahara yao kati ya tarehe 20 na 24 ya kila mwezi," amesema Dk. Kijaji.

Wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge huyo, Dk. Kijaji amesema mshahara ni mali ya mtumishi na anaweza kuutumia anavyotaka ikiwa ni pamoja na kuwekeza na kwamba, Serikali imekuwa ikitenda haki kwenye kuwapandisha madaraja watumishi.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi