loader
Picha

Mwakinyo atikisa Dodoma, wabunge kumchangia Sh milioni 7.8

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekubaliana kuchanga sh 20,000/- kila mmoja wao kwa lengo la kumpongeza bondia Hassan Mwakinyo.

Endapo wabunge wote, takribani 393, watatoa kiasi hicho walichokubaliana, mwanamasumbwi huyo ataondoka na kitita cha sh mil 7.8/- kama zawadi.

Mwakinyo aliweka historia mpya katika ngumi mwisho wa wiki iliyopita, baada ya kumchapa mpinzani wake Sam Eggington wa Uingereza kwa ‘Technical Knock Out’ (TKO).

Hoja ya kumchangia Mwakinyo ilitolewa na mmoja ya wabunge na kuungwa mkono na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akihitimisha Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 12 wa Bunge.

Spika Job Ndugai alipohoji wabunge kama wanaridhia, walikubali bila kupinga huku baadhi wakisema kiasi hicho ni kidogo.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi