loader
Picha

Serikali: Mwenge hautumii fedha nyingi na hautokaa makumbusho

Serikali imesema si kweli kwamba Mwenge wa Uhuru unatumia fedha nyingi za walipa kodi na haioni umuhimu wa kuuweka Makumbusho ya Taifa.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde amesema bungeni kuwa, hoja ya gharama kubwa wakati wa mbio za mwenge si ya msingi hasa ukizingatia kiasi cha fedha zinazotumika na thamani ya miradi inayozinduliwa.

"Kwa mfano; mwaka 2017 Serikali ilitenga shilingi milioni 463 kugharamia shughuli za Mwenge wa Uhuru. Ukilinganisha kiasi hicho na miradi ya maendeleo 1,512 iliyozinduliwa yenye thamani ya shilingi trilioni 1.1 ni dhahiri kuwa hoja ya gharama kwa kubwa sio ya msingi" amesema Mavunde.

Ameyasema hayo wakati anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Zubeda  Hassan Sakuru.

Mbunge huyo alitaka kufahamu kama Serikali haioni umuhimu wa kurudisha Mwenge wa Uhuru Makumbusho ya Taifa na kuzifuta sherehe za mwenge kwa kuwa zinatumia fedha nyingi za walipa kodi wakati Watanzania wengi wana maisha duni.

Ametaja miongoni mwa sababu za kutouweka mwenge Makumbusho ya Taifa kuwa ni kuutumia kuchochea maendeleo na kwamba, katika miaka mitano iliyopita, miradi 6,921 yenye thamani ya shilingi trilioni 2.5 ilizinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi.

 

"Mbio za Mwenge wa Uhuru huwakumbusha Watanzania falsafa nzito ya Mwenge wa Uhuru inayotoa taswira ya Taifa ambalo waasisi wetu walitaka kulijenga Taifa lenye amani, linalojitegemea na lenye kuheshimu misingi ya utu na usawa wa binadamu"amesema Mavunde.

Amesema, Mwenge wa Uhuru pia unaimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwa huzungushwa Tanzania bara na Zanzibar na pia wanaoukimbiza wanatoka sehemu zote mbili za muungano.

TANZANIA na Uganda zimeanzisha rasmi Jukwaa la Biashara baina ya ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi