loader
Picha

Waziri: JWTZ itaendelea kulinda amani

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imesema imesema askari wa Tanzania wanakwenda kwenye nchi mbalimbali kulinda amani na si kushiriki kwenye mapigano.

Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hussein Mwinyi amesema bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa kuwa Tanzania ina wajibu wa kulinda amani kwenye nchi hizo kwa kuwa ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya za kikanda za EAC, SADC na jumuiya ya nchi za maziwa makuu.

Ameyasema hayo wakati anajibu swali la Mbunge wa Bumbwini, Muhammed Amour Muhammed. 

Mbunge huyo alitaka kufahamu mtazamo wa Serikali kuhusu askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaokwenda kwenye maeneo yenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na wanapoteza maisha.

Waziri Mwinyi amesema, Tanzania itaendelea kushiriki kulinda amani katika nchi mbalimbali ili kutimiza wajibu kimataifa na itachukua tahadhari kuepuka maafa yaliyowahi kutokea.

"Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limechukua hatua ya kutoa mafunzo ya kutosha kwa vikosi vyetu vinavyopewa jukumu hili pamoja na kuwaongezea vifaa vua kisasa ili waweze kujilinda dhidi ya mashambulio ya vikundi vya waasi," amesema.

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kutowachagua wagombea uongozi katika Uchaguzi ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi