loader
Picha

Serikali yasema haikusudii kuunganisha Elimu ya Msingi, VETA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema, mitaala ya elimu ya ufundi lazima izingatie mazingira ya mahali husika.

Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Joyce Ndalichako pia amesema, Serikali itaendelea kutoa elimu ya msingi kwa miaka saba na haitaunganishwa na mafunzo ya ufundi stadi.

"Masuala ya ufundi yanatakiwa yaangalie mazingira halisi ya mahali ufundi unapofanyika. Kwa hiyo suala la kuangalia masuala ya gesi au masuala ya uvuvi ndiyo jambo ambalo limekuwa likifanyika..

"Kwa hiyo niendelee kutoa wito kwa wote wanaotoa mafunzo ya ufundi stadi wahakikishe kwamba mitaala yao inazingatia mazingira halisi ya pale ambako wanatoa mafunzo ili kuwawezesha wananchi wa eneo husika kuongeza tija katika shughuli wanazozifanya"amesema Waziri Ndalichako.

Amewaeleza wabunge kuwa, shule saba za ufundi za kitaifa zimeboreshwa ikiwa ni pamoja na kupewa vifaa vya karakana, na pia Serikali ipo tayari kuruhusu shule za sekondari zinazokidhi vigezo kwenye Halmashauri ziwe za ufundi.

Amesema, elimu ya msingi haitaunganishwa na ufundi kwa sababu maudhui kwenye mtaala wa elimu ya msingi yanakidhi mahitaji ya wahitimu wa ngazi hiyo ya elimu.

"Na vilevile muda ambao mwanafunzi wa elimu ya msingi wanakaa shuleni hauwezi kutosha kuunganisha na mafunzo ya ufundi stadi. Hivyo, mafunzo ya ufundi stadi yataendelea kutolewa na Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA)"amesema Profesa Ndalichako.

TANZANIA na Uganda zimeanzisha rasmi Jukwaa la Biashara baina ya ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi